Tafuta katika Blogu Hii

Jumanne, 30 Januari 2018

BARAZA LA MADIWANI



Manispaa ya Temeke yafanya Baraza la madiwani leo katika ukumbi wa Iddi Nyundo uliopo ndani ya manispaa.Akizungumza katika baraza la madiwani kuanza Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mh:Felix Lyaniva alikumbusha watendaji pamoja na madiwani kusimamia sera ya elimu bure katika kata zao. Aliwataka kuelimisha umma kuwa elimu bure inawezekana kama dhamira ya serikali ya awamu ya tano ya Dr John Pombe Magufuli inavyokazana kulitekeleza hilo.



Pia amewaasa wakuu wa shule ambao wanavunja sheria ya kuchukua tozo yoyote ya kielimu kuacha mara moja. Pia aliwapongeza madiwani wote kwa namna wanavyotekeleza sheria za utawala bora.Na aliwataka madiwani kuhakikisha makusanyo ya kodi yanapatikana kulingana na makadirio ya bajeti ya Halmashauri.Kisha akawatakia kikao kizuri chenye mafanikio.




Mstahiki Meya Abdallah Chaurembo alimpongeza Mh: Lyaniva,juhudi zake kuhimiza maendeleo na akahaidi kuyafanyia kazi. Madiwani walipokea taarifa za utekelezaji kazi kutoka katika kata kwa kipindi cha robo ya pili Oktoba-Disemba,2017. Taarifa hizo zilijadiliwa kwa kina ikiwemo miradi ya maendeleo inayoendelea katika kata na ile ambayo imekwisha kukamilika. Hata hivyo baraza lilijadili makusanyo ya kodi katika kila kata ambapo kata ya Kilungule chini ya diwani Said Fella imeongoza katika ukusanyaji wa kodi.




Pia makusanyo ya huduma ya uzoaji taka kata ya Yombo Vituka yalipanda na kufikia kiasi cha sh:36,822,350.00 na kupongezwa na madiwani.
Hata hivyo Baraza la madiwani lilidhibitisha mihtasari ya mikutano ya Halmashauri na vikao vya kamati za kudumu katika robo ya pili kwa kipindi cha Oktoba-Disemba 2017.



Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke Ndug:Nasibu Mmbaga aliwakumbusha watendaji kufanya kazi kwa juhudi katika kuhakikisha wanajikita katika kuboresha na kuwekeza sector ya elimu na afya. Katika robo ya pili ya bajeti manispaa imeweza kujenga matundu 98 ya vyoo,madawati 110,000 na madarasa 480 katika shuletofauti.Aitha, shilingi milioni 400 zimetengwa kwaajili ya marekebisho na ujenzi wa miundo mbinu ya afya na elimu katika kata za Yombo Vituka na Kata ya Sandari.Pia Mkurugenzi Mmbaga alisisitiza utumiaji wa force account ili kupunguza gharama katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.Alitoa mfano wa ujenzi wa daraja la Kibonde maji ambalo limejengwa kwa mfumo huo.





Mstahiki Meya akiahirisha kikao amewaagiza watendaji wa kata na mitaa kusimamia ukusanyaji wa kodi, ili kuleta maendeleo ya haraka ndani ya Manispaa.












Jumatano, 17 Januari 2018

VIFO VYA MAMA NA MTOTO ITAKUWA HISTORIA TEMEKE


Halmashauri inatarajia kujenga jengo la upasuaji,wodi ya wazazi na mtoto, ukarabati na ujenzi wa Maabara pamoja na vyumba vya watumishi katika kituo cha afya Yombo Vituka na Zahanati ya Majimatitu ikiwa na lengo la kuimarisha afya ya mama na mtoto pia kupunguza vifo vitokanayo na uzazi.

Ujenzi huu unatarajia kukamilika ifikapo mwezi April na utagharimu jumla ya Shilingi Milioni mia nane(800) ambapo kituo cha afya Yombo Vituka kitagawiwa kiasi cha Shilingi Millioni Mia nne (400) na Zahanati ya Majimatitu Shilingi Millioni mia nne(400).

Akizungumza na wafanyakazi wa kituo cha afya Yombo Vituka wakati wa ziara ya kuangalia matumizi ya fedha zilizotolewa na Benki ya Dunia, Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bibi Dorothy Mwaluko aliwapongeza sana watumishi wa Zahanati hiyo pamoja na Kamati mbalimbali, kwa kujitoa kwao na kuhakikisha ujenzi unatekelezeka bila kuwa na malalamiko wala migongano. Pia uwazi umeonekana wa hali ya juu na kuwashauri waendelee na ushirika hou.


Naye Mwita Waibe kutoka Idara ya Afya, ustawi wa jamii na Lishe Tamisemi alisisitiza kuwa Ofisi yake inatarajia kuona ujenzi huo unakamilika ndani ya muda uliopangwa ili kuleta tija na kuendana na malengo ya mradi huo.Pia alisisitiza kuwa miradi hii itajengwa na kusimamiwa na kituo hivyo kusisitiza kuchagua mafundi wenye uwezo ambapo itapelekea thamani ya fedha iendane na ujenzi husika.


Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri Bw. Primy Damas aliwahakikishia wajumbe toka Tamisemi kuwa mpaka kufikia mwezi Aprili 2018, ujenzi utakuwa umekamilika na kuanza kutumika.

Timu hiyo ya ukaguzi pia iliongea na watumishi wa kusikiliza kero zao ikiwemo za malimbikizo ya madeni mbalimbali na kuahidi kuzifanyia kazi na nyingine kuwasilisha eneo husika kwa utatuzi zaidi.

Alhamisi, 11 Januari 2018

TEMEKE YAZIDI KUNG'AA KWENYE MIRADI YA MAENDELEE



Wakuu wa idara na vitengo wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke wafanya  ukaguzi wa miradi ya maendeleo yenye thamani ya zaidi ya bilioni 3. 



Miradi ambayo inajengwa na vyanzo vya mapatao vya halmashauri ya manispaa yaTemeke. Ambapo mradi wa kisima cha maji kata ya Azimio mtaa wa Mbuyuni wenye thamani ya zaidi ya milioni 400 umefadhiliwa na Benki ya Dunia umefikia hatua za mwisho ili wananchi waanze kupata huduma ya maji.




Miradi hiyo ambayo imetembelewa ni ujenzi wa vyumba 6 vya madarasa Chamazi sekondari, ujenzi wa vyumba 2 vya madarasa shule ya Msingi Mgeninani, Ukaguzi wa Zahati ya Kijichi, ujenzi wa vyumba 4 vya madarasa shule ya sekondari Mbagala, ukaguzi wa zahanati Yombo vituka, ujenzi wa vyumba 2 vya madarasa s/Msingi Karume, kukagua mradi wa maji Mabatini, ujenzi wa vyumba 4 vya madarasa Miburani sekondari.




Mradi wa vyumba vya madarasa katika shule ya karume na shule ya Msingi  Mgeninani imekamilika.






Miradi yote ipo katika hatua nzuri ili kukamilika. 










TEMEKE BILA UCHAFU INAWEZEKANA.

MKUU WA WILAYA YA TEMEKE APOKEA MAPIPA ZAIDI YA 241 KWA AJILI YA KAMPENI YA “TEMEKE BILA UCHAFU INAWEZEKANA” Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mh F...