Tafuta katika Blogu Hii

Jumapili, 7 Oktoba 2018

Tuige mfano wa Chaurembo


Wito huu umetolewa na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM, Wilaya ya Temeke Ndugu: AL Mish Hazal na kutaka Madiwani wote wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Temeke Kuiga mfano wa Mh: Chaurembo, ambaye ni Mstahiki Meya wa Manispaa ya Temeke na Diwani ya kata ya Charambe, kwa kazi nzuri aliyoifanya ya kutoa Semina elekezi kwa mabalozi wa mashina alisema "semina hizi ziende kwenye kata zote za Wilaya ya Temeke".
Akitoa salamu za utangulizi, Ndugu AL Mish, alimpongeza Mh: Chaurembo leo October 07, 2018 katika semina ya mabalozi wa mashina 63 kata ya Charambe katika Ukumbi wa Iramba na kusisitiza kuwa Mstahiki anafaa kuigwa kwa kazi nzuri anazofanya.
"Ninafahamu ya kwamba Charambe ni ngome ya CCM, Mh: Chaurembo ambaye ni Diwani wenu anafanya kazi kubwa sana, Ninafuraha sana kuona na kusikia hali ya siasa katika eneo la Charambe ipo imara...
Kazi kubwa imefanyika kukiimarisha Chama,hongera sana Mh: Chaurembo."
Akigusia mchango na umuhimu wa mabalozi wa mashina katika kukiimarisha Chama cha Mapinduzi CCM, Ndugu AL Mish alisema "Mimi nimekuwa nikiguswa sana na mabalozi wa mashina, mabalozi ni chachu ya ustawi wa chama, nitaendelea kuwaunga mkono na kushirikiana nao katika kukiimarisha chama"alisisitiza.
Ndugu AL Mish aliwasihi mabalozi hao wa mashina wanapofanya vikao vyao vya dharura wampatie mwaliko ili aweze kuona jinsi gani wanavyoendesha vikao.
Vile vile aliwataka waweze kutafakari maelekezo wanayopewa na viongozi wao, Pia wawe na mikakati mizuri ya kuhakikisha Chama cha Mapinduzi CCM kinaibuka na ushindi katika chaguzi za Serikalk za mitaa 2019.
AL Mish aliwataka mabalozi hao wa mashina wawe makini na Wanachama mamluki wanaokuja kujiandikisha na kujifanya ni wana CCM.
Mwisho ndugu AL Mish Hazal aliwataka mabalozi wa mashina wawe na mfuko wa fedha pia wawe na sera ya uwekezaji.
alitoa wito kwa wanachama wa CCM kujichangisha fedha na kuweka kwenye mfuko wa fedha ili chama kiweze kujitegemea katika chaguzi mbalimbali.

Soma Magazeti ya Leo Jumatatu 8/10/2018

SOMA MAGAZETI YA LEO JUMATATU 08/10/2018



Alhamisi, 4 Oktoba 2018

Maafisa afya wapokea mafunzo kuhusu Ebola



Maafisa afya wote wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke wamehudhuria mafunzo ya namna ya kujikinga na ugonjwa wa Ebola. Mafunzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa Iddi Nyundo uliopo Manispaa,yaliyoendeshwa na wataalamu kutoka Ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam wakishirikiana na wataalamu kutoka Wizara ya Afya.



Mafunzo hayo yenye lengo la kuwajengea uwezo wataalamu wote wa afya wa Halmashauri ili kukabiliana na ugonjwa huo endapo utatokea.
Mtaalamu kutoka Wizara ya Afya na maendeleo ya jamii kitengo cha Epidermiology Bib:Vida Mmbaga, ambae alifundisha mambo mbalimbali ikiwemo jinsi ya kujikinga, kumtambua mgonjwa na namna ya kumuhudumia mgonjwa wa Ebola.Aliwaambia wataalamu hao ni muhimu kuwa na vikao mbalimbali vya ndani ili kujadili namna ya kujipanga kutokomeza virusi hivyo, ikiwemo kujiandaa na vifaa na eneo maalaumu la kumuhudumia mgonjwa mwenye dalili zitokanazo na ugonjwa huo endapo ugonjwa huo ukitokea. Pia aliwakumbusha maafisa afya kuendelea kujifunza juu ya kuukabili ugonjwa huo kwa kupata mafunzo ya mara kwa mara.




Hata hivyo mafunzo hayo yataendelea kwa ngazi zote za Halmashauri mpaka kumfikia mwananchi wa ngazi ya chini anayeishi Temeke.




Ebola ni ugonjwa unaosababishwa na virusi vya homa ya hemoraji (kumwaga damu kwa sana). Kati ya watuu 10 waliopata virusi vya ebola,wastani kati ya watu 5 na 9 hufa.Imeonekana kuwa nchi za jirani na Tanzania zimekutwa na wagonjwa wenye virusi hivyo.

TEMEKE BILA UCHAFU INAWEZEKANA.

MKUU WA WILAYA YA TEMEKE APOKEA MAPIPA ZAIDI YA 241 KWA AJILI YA KAMPENI YA “TEMEKE BILA UCHAFU INAWEZEKANA” Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mh F...