Tafuta katika Blogu Hii

Jumatano, 21 Septemba 2016

TEMEKE KUPANDA MITI ZAIDI YA 12000 OCTOBA MOSI

     Mkuu wa Mkoa wa Dar-es-Salaam Bw.Poul Makonda amefanya ziara ya ukaguzi wa maeneo yaliopo katika Wilaya ya Temeke ambayo yatahusika katika zoezi zima la upandaji wa miti mnamo tarehe 1 ya Mwezi wa 10.
Bwana Makonda amesema zoezi hilo ni la Mkoa mzima wa Dar-es-salaam na anawaomba wananchi wa Mkoa wa Dar-es-salaam kujitokeza kwa wingi ili kushiriki katika zoezi hilo.
Nae Mkuu wa wilaya ya Temeke Bw Felix Jackson Lyaniva amesema Temeke inatarajia kupanda miti zaidi ya elfu kumi na mbili katika siku hiyo.Lyaniva amesema Temeke imejipanga kuhakikisha zoezi hilo linafanikiwa kwa asilimia kubwa pia Mkuu wa wilaya amewaomba wananchi wa Temeke kuhakikisha wanashiriki zoezi hilo kwa walau kila mkazi wa Temeke kuhakikisha anapanda miti walau miwili katika mazingira ya nyumba anayoishi.   

TEMEKE BILA UCHAFU INAWEZEKANA.

MKUU WA WILAYA YA TEMEKE APOKEA MAPIPA ZAIDI YA 241 KWA AJILI YA KAMPENI YA “TEMEKE BILA UCHAFU INAWEZEKANA” Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mh F...