Shule hii ilianzishwa mwaka 2006 ikiwa na vyumba viwili tu vya madarasa,na tangu kuanzishwa kwa shule hii imekuwa mkombozi kwa wanafunzi wengi wanaotoka maeneo ya Mbagala,Kigamboni,Kongowe,na sehemu nyingine tofauti za Manispaa ya Temeke.kitengo cha Habari na Mahusiano cha Manispaa ya Temeke kilifika shuleni hapo ili kuweza kutambua changamoto zinazopatikana shuleni hapo.
Changamoto kubwa ambayo wanafunzi wengi wa shule hiyo waliizungumzia sana ni Usafiri wa kufika shuleni hapo kwa wanafunzi wanakaa maeneo ya Mbagala wanafunzi hao walisema hulazimika kutembea umbali wa kilometa 13 kila siku asubuhi jambo ambalo huwafanya wafike shuleni wakiwa wamechelewa na hivyo kukosa baadhi ya vipindi hasa vipindi vya asubuhi,na wengine hulazimika kupanda malori ya Mchanga ambayo huelekea katika machimbo ya mchanga yaliyopo katika maeeneo ya Kisarewe ii Jambo ambalo huatarisha maisha yao hasa kwa watoto wakike ambao wao wamedai hukutana na changamoto zaidi wanapopanda malori hayo kwani kuna baadhi ya Madereva ama Matingo wa malori hayo ambao si wastaarabu huwaomba namba za simu na wengine hukataa kuwashusha mpaka wawaachie namba za simu.Ili kukabiliana na Changamoto hiyo uongozi wa shule hiyo ukishirikiana na TASAF ulifanikiwa kujenga bweni la Wasichana,lakini bado tatizo hilo limeendelea na hii imetokana na ongezeko la wanafunzi shuleni hapo hivyo shule kushindwa kuwaweka wanafunzi wote katika bweni hilo kutoka na udogo wa bweni hilo.
Majengo ya Madrasa Shule ya Sekondari Kisarawe ii |
Jengo la bweni la Wasichana la Shule ya Sekondari Kisarawe ii. |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni