Halmashauri ya Manispaa ya Temeke yakabidhiwa mabenchi kutoka kampuni ya Goodone,mabenchi hayo yalipokelewa na katibu tawala wilaya Mh Hashim Komba ambapo amepokea mabenchi 30 kwa ajili ya matumizi ya wagonjwa hususani wajawazito katika kitengo cha huduma ya uzazi, mama na mtoto katika hospitali ya Mbagala Rangi tatu na Kampuni ya Goodone. Aidha misaada hiyo imelenga pia kusaidia kituo cha afya kata ya Yombo, hospitali ya Yombo vituka.
Sambamba na hilo, kampuni ya Goodone imetoa sabuni za kufulia mashuka ya hospitali hizo. Misaada hiyo imegharimu jumla ya Tsh Milioni 12.
Mganga Mfawidhi wa hospitali ya Mbagala Rangi Tatu DK. Joseph Kaini amewashukuru wadau wote na mkurugenzi Mkuu wa Goodone ambaye ameonyesha nia ya kusaidia zaidi hospitali..
Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya GOODONE |
Mabenchi yaliyotolewa na kampuni ya GOODONE |
Mganga mfawidhi Dk.Joseph Kaini akizungumza na uongozi wa GOODONE |
Mh DAS akipokea moja kati ya mabenchi yaliyotolewa na kampuni GOODONE (katikati),Mr.WU mkurugenzi mkuu GOODONE(kushoto) Dr.Joseph kain(kulia) |
Mh DAS akitoa shukrani kwa uongozi wa kampuni ya GOODONE kwa niaba ya wananchi |
Miongoni mwa msaada wa sabuni zilizotolewa na GOODONE |
Wananchi wa Mbagala wakijitokeza kupokea misaada hiyo |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni