Mkuu wa Wilaya ya
Temeke Mh Felix Lyaniva leo amepokea
mapipa zaidi ya 241 kutoka katika
kampuni ya Sigara TCC kwa ajili ya usafi wa Mazingira kupitia Kampeni ya “
Temeke bila Uchafu inawezekana” yenye kulenga kuweka Mazingira nadhifu katika
Wilaya ya Temeke.
Mhe. Mkuu wa Wilaya ya Temeke Felix Lyaniva mwenye suti nyeupe akiwa ameshika pipa akimkabidhi rasmi kaimu Mkurugenzi kwa ajili ya kuwakabidhi watendaji wa Kata na Mitaa tayari kwa matumizi. |
Akitoa taarifa mbele ya
mgeni rasmi mwakilishi wa TCC Bi Neema alisema Kampuni ya Sigara TCC imekuwa
mdau mkubwa wa maendeleo katika Mikoa mbalimbali yaTanzania ikisaidia makundi
mbalimbali ya kijamii mfano walemavu,Wazee, Wajasiriamali,Wasanii,na Nyanja ya
Mazingira.
Lakini siku ya leo TCC imeandaa
mapipa 241 kwa ajili yaUstawishaji
wa Mazingira kupitia kampeni ya “Temeke bila uchafu inawezekana”. Mapipa hayo
yote ni salama kwa matumizi kwa kuwa awali yalikuwa yanatumika kwa ajili ya
kuhifandhi gundi na gundi hiyo haina kemikali ambayo inaweza
kuathiri afya za jamii wakati wa matumizi ya kutupa taka.
“Tunakabidhi mapipa 241 tutaendelea kutoa mapipa 50 kila mwenzi kwa Wilaya ya Temeke
hadi tutakapoona yamekidhi mahitaji ndipo sasa tutaenda katika Wilaya zingine
za Mkoa wa Dar es Salaam, tunafanya hivyo kwa kuwa Kampuni ya TCC ipo Wilaya ya
Temeke”, Alisema Bi Neema.
Aidha Mkuu wa Wilaya ya
Temeke Mh Lyaniva wakati
akikabidhiwa mapipa hayo amesema anaishukuru Kampuni ya Sigara TCC kwa kuamua
kuunga mkono juhudi za usafi wa Mazingira katika Wilaya ya Temeke na kutoa rai
kwa Makampuni mengine ndani ya Wilaya ya Temeke kuiga mfano wa TCC.
Mkuu wa Wilaya Temeke Mh Felix Lyaniva mwenye suti nyeupe akifurahia jambo baada ya kupokea mapipa 241 kutoka TCC katika viwanja vya TCC club Chang'ombe. |
“Wilaya ya Temeke
imejipanga katika kuboresha ustawi wa watu wake na nmna pekee ni kuhakikisha
jamii ya Temeke inaishi katika mazingira nadhifu na salama yenye kuvutia, ni wahakikishie TCC madumu mnayonikabidhi
mimi na pokea lakini nakabidhi yote kwa watendaji wa Mitaa na Kata na bahati
nzuri wote wapo hapa” alisema Mh
Lyaniva.
Amehitimisha kwa
kuwataka watu na wadau mabalimbali kuendelea kutunza mazingira kwa kuyaweka
katika hali ya usafi na kupanda miti ya matunda ambayo itakuwa na faida zaidi
ya moja pia ameitaka TCC kufufua eneo la TCC
Club iwe sehemu nzuri ambayo wananchi watajipatia burudani na nyama choma,
maagizo ambayo TCC wamekubali na kuhaidi kulifanyia kazi mapema iwezekanavyo .
# Temeke bila uchafu inawezekana.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni