Tafuta katika Blogu Hii

Jumatano, 14 Agosti 2019

UTALII WA NDANI UNAANZA NA WEWE.

Hii ni kauli ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke ndugu Lusubilo J Mwakabibi, aliyoitoa leo alipotembelea hifadhi ya wanyama ya Mikumi akiongozana na waheshimiwa Madiwani pamoja na timu ya watendaji wa Manispaa hiyo.

Mwakabibi alisema Watanzania tujifunze utamaduni wa kutembelea mbuga zetu, maana haiwezekani watalii toka nje ya nchi waje kutembea na kujionea vivutio na sisi tupo hapahapa nchini tunashindwa kufanya utalii wa ndani.

"Hakuna miujiza mingine zaidi ya kuamua, maamuzi sahihi na kujipanga ndio msingi wa kupata yote haya.Watanzania tuwe na tabia ya kutunza fedha kwaajili ya kufanya matukio kama haya hata mara moja kwa mwaka inasaidia kuimarisha afya ya akili na kuwa na ari ya kuitangaza nchi yetu vema ndani na nje ya mipaka ya Tanzania" alisema Mwakabibi.

Alifafanua zaidi kwamba tunamaeneo mengi ya utalii kuanzia kaskazini mwa nchi mpaka kusini mashariki mpaka magharibi, ni kiasi cha kuamua tu kwamba sasa tunaamka kutembelea vivutio vyetu na kufuta mawazo ya kuwa utalii unafanywa na watu wa mataifa ya nje.

Sambamba na hilo Mh. Hemed Karata alisema amefurahishwa sana na utalii huo kwani anaimani baada ya hapa watendaji pamoja na Waheshimiwa Madiwani watakuwa mabalozi wazuri wa kuitangaza nchi yetu.

Ninaimani sisi ni mabalozi wazuri wa nchi na kwa familia zetu, leo tumejionea vivutio vingi sana na kupata maelezo ya wanyama mbalimbali ambayo yanaleta hamasa na mwamko wa kutamani kutembelea vivutio vyote vya nchi. Alisema Mh.Karata.

Pamoja na hayo timu ya utalii ilipata fursa ya kutanabishwa masuala mbalimbali ya utalii na kujuzwa asili ya neno Mikumi lilitokana na aina ya miti ya "mikoche" (kwa lugha ya vidunda na wasagara) na kwamba, endapo miti hiyo ikiwa mingi zaidi huitwa mikumi.

Alifafanua zaidi kwamba watu wapende utalii wa ndani kwa kuwa hata lugha inayotumika ni rafiki kwakuwa ni lugha mama ya Taifa la Tanzania.

Hifadhi ya wanyama ya Mikumi inaukubwa wa kilometa 3,230 na inapatikana barabara kuu ya kuelekea Iringa,ina wanyama wa aina tofauti ambao uhama toka hifadhi ya Selous na kuhamia Mikumi kisha kurejea Selous tena.

TEMEKE WAPITIWA MAFUNZO YA ITIFAKI NA DIPLOMASIA.

Wakuu wa Idara na Vitengo toka Manispaa ya Temeke wamepatiwa mafunzo ya Iti
faki na Diplomasia. Mafunzo hayo yalifanyika katika ukumbi wa Stella Maris uliopo Bagamoyo mkoani Pwani. Lengo la mafunzo hayo ni kuwaongezea uwezo katika masuala ya kidiplomasia na itifaki.
Mafunzo hayo yaliongozwa na wakufunzi toka katika chuo cha Diplomasia kilichopo Dar-es-salaam.

Jumamosi, 3 Agosti 2019

Waziri wa Mifugo na Uvuvi atemebelea Banda la Manispaa ya Temeke katika maonyesho ya nanenane.

Ikiwa ni siku ya tatu toka kuanza kwa maonesho ya nanenane yanayofanyika kila mwaka,Manispaa ya Temeke imepata ugeni kwa kutembelewa na waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh.Luhaga MPina ambae alitembelea banda la manispaa ya Temeke kwenye maonesho ya nanenane mkoani Morogoro na kuvutiwa namna wajasiriamali wa Temeke wanavyotengeneza bidhaa zao ,hivyo aliwasihi waendelee kuongeza juhudi katika shughuli zao wanazozifanya ili kuweza kujikwamua kiuchumi.pia mbali na waziri huyo ,wakazi mbalimbali wa mkoani humo wameweza kutembelea banda la Manispaa ya Temeke katika maonesho hayo.



Maajabu katika ufugaji wa samaki ni katika banda la Manispaa ya Temeke.

TEMEKE BILA UCHAFU INAWEZEKANA.

MKUU WA WILAYA YA TEMEKE APOKEA MAPIPA ZAIDI YA 241 KWA AJILI YA KAMPENI YA “TEMEKE BILA UCHAFU INAWEZEKANA” Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mh F...