Tafuta katika Blogu Hii

Jumatatu, 16 Desemba 2019

TEMEKE BILA UCHAFU INAWEZEKANA.

MKUU WA WILAYA YA TEMEKE APOKEA MAPIPA ZAIDI YA 241 KWA AJILI YA KAMPENI YA “TEMEKE BILA UCHAFU INAWEZEKANA”
Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mh Felix Lyaniva leo amepokea mapipa zaidi ya 241 kutoka katika kampuni ya Sigara TCC kwa ajili ya usafi wa Mazingira kupitia Kampeni ya “ Temeke bila Uchafu inawezekana” yenye kulenga kuweka Mazingira nadhifu katika Wilaya ya Temeke.

Mhe. Mkuu wa Wilaya ya Temeke Felix Lyaniva  mwenye suti nyeupe akiwa ameshika pipa akimkabidhi rasmi kaimu Mkurugenzi kwa ajili ya kuwakabidhi watendaji wa Kata na Mitaa tayari kwa matumizi.
Makabidhiano ya Mapipa au madumu  hayo ya taka yamefanyika katika viwanja vya TCC Chang’ombe Wilaya ya   Temeke Jijini Dar es Salaam, na kuhudhuriwa na timu ya Wafanyakazi wa TCC, Watendaji Kata na Mitaa,Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya, Katibu Tawala Wilaya ya Temeke, Mkurugenzi wa Manispaa ,Wananchi  na baadhi ya wataalam wa Manispaa ya Temeke.

Akitoa taarifa mbele ya mgeni rasmi mwakilishi wa TCC Bi Neema alisema Kampuni ya Sigara TCC imekuwa mdau mkubwa wa maendeleo katika Mikoa mbalimbali yaTanzania ikisaidia makundi mbalimbali ya kijamii mfano walemavu,Wazee, Wajasiriamali,Wasanii,na Nyanja ya Mazingira.
Lakini siku ya leo TCC imeandaa mapipa 241 kwa ajili yaUstawishaji wa Mazingira kupitia kampeni ya “Temeke bila uchafu inawezekana”. Mapipa hayo yote ni salama kwa matumizi kwa kuwa awali yalikuwa yanatumika kwa ajili ya kuhifandhi gundi na gundi hiyo haina kemikali ambayo   inaweza kuathiri afya za jamii wakati wa matumizi ya kutupa taka.
“Tunakabidhi mapipa 241 tutaendelea kutoa mapipa 50 kila mwenzi kwa Wilaya ya Temeke hadi tutakapoona yamekidhi mahitaji ndipo sasa tutaenda katika Wilaya zingine za Mkoa wa Dar es Salaam, tunafanya hivyo kwa kuwa Kampuni ya TCC ipo Wilaya ya Temeke”, Alisema Bi Neema.
Aidha Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mh Lyaniva wakati akikabidhiwa mapipa hayo amesema anaishukuru Kampuni ya Sigara TCC kwa kuamua kuunga mkono juhudi za usafi wa Mazingira katika Wilaya ya Temeke na kutoa rai kwa Makampuni mengine ndani ya Wilaya ya Temeke kuiga mfano wa TCC.

Mkuu wa Wilaya Temeke Mh Felix Lyaniva mwenye suti nyeupe akifurahia jambo baada ya kupokea mapipa 241 kutoka TCC katika viwanja vya TCC club Chang'ombe.

“Wilaya ya Temeke imejipanga katika kuboresha ustawi wa watu wake na nmna pekee ni kuhakikisha jamii ya Temeke inaishi katika mazingira nadhifu na salama yenye kuvutia,  ni wahakikishie TCC madumu mnayonikabidhi mimi na pokea lakini nakabidhi yote kwa watendaji wa Mitaa na Kata na bahati nzuri wote wapo hapa” alisema Mh Lyaniva.
Amehitimisha kwa kuwataka watu na wadau mabalimbali kuendelea kutunza mazingira kwa kuyaweka katika hali ya usafi na kupanda miti ya matunda ambayo itakuwa na faida zaidi ya moja pia ameitaka TCC kufufua eneo la TCC Club iwe sehemu nzuri ambayo wananchi watajipatia burudani na nyama choma, maagizo ambayo TCC wamekubali na kuhaidi kulifanyia kazi mapema iwezekanavyo .
# Temeke bila uchafu inawezekana.

TEMEKE BILA UCHAFU INAWEZEKANA.

MKUU WA WILAYA YA TEMEKE APOKEA MAPIPA ZAIDI YA 241 KWA AJILI YA KAMPENI YA “TEMEKE BILA UCHAFU INAWEZEKANA” Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mh F...