Mbaga alieleza kuwa kuna maeneo matano ambayo yametengwa rasmi kwa ajili ya biashara kama vile Soko la Toangoma, Sigara, Kiponza na Makangarawe, maeneo hayo yakiwa na huduma zote za kijamii ikiwepo vyoo bora.
Maafisa Afya wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke wakiwa kwenye ukaguzi wa wafanya bisahara ya vyakula katika kituo cha Mabasi cha Mbagala Rangi Tatu.(picha na Mathew Jonas) |
Aliongeza kuwa Halmashauri imetenga maeneo kwa ajili Masoko ikiwa ni pamoja na Temeke stereo, Vetenari Tazara, Madenge, Tandika kuu, Tandika Kampochea, Keko Magurumbashi, Temeke mwisho, Bulyaga, Kizuani, Zakheem, Mbagala rangi, Mtoni Mtongani, Lumo,Urassa, Feri, Maguruwe,Kabuma na Limboa.
Pia Mkurugenzi aliongeza kuwa Halmashauri imekua ikifanya jitahada za wazi za kuimarisha usafi wa mazingira ya stendi ya Mbagala rangi tatu kwa kufanya ukaguzi wa mara kwa mara ili kuhakikisha eneo hilo pamoja na maeneo yanayozunguka yanakuwa katika hali ya usafi ili kuwa epusha wananchi na magonjwa ya milipuko haswa kipindupindu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni