Tafuta katika Blogu Hii

Ijumaa, 28 Oktoba 2016

MKUU WA WILAYA YA TEMEKE AAINISHA MAENEO RASMI YA KUFANYIA BIASHARA.

Mkuu wa wilaya ya Temeke Bw. Felix Jackson Lyaniva ameainisha maeneo rasmi ya kufanyia biashara ndogondogo na kuwataka wafanyabiashara wadogowadogo maarufu kama wamachinga wanaofanya biashara zao nje ya maeneo rasmi kuhamia na kufanyia biashara katika maeneo yafuatayo


Mkuu wa Wilaya ya Temeke Bw.Felix Jackson Lyaniva.

Toangoma kata ya Toangoma, Kilamba kata ya Charambe, Kiponza kata ya Chamazi, Kibondemaji kata ya kibondemaji, Mangaya kata ya Chamazi(Mwembe Pacha), Makangarawe kata ya Makangarawe, Buza kata ya Buza na Sigara lililopo kata ya Yombo Vituka. 

Jumamosi, 1 Oktoba 2016

Makamu wa Rais ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan amezindua rasmi Kampeni ya Mti wangu.
Uzinduzi huo umefanyika katika Barabara ya Kilwa wilayani Temeke.
Katika uzinduzi huo Makamu wa Rais amesema kila mmoja wetu ana jukumu la kupanda miti na kuitunza ili kuweza kuhifadhi mazingira pamoja na kukabiliana na mabadilko ya tabia ya nchi pamoja na mabadiliko ya hali ya hewa kwa ujumla.
Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan akizungumza na wananchi kaika  Uzinduzi Kampeni ya Mti wangu uliofanyika katika Barabara Kilwa Temeke. 
 Ameongeza kwa kusema kuwa Mazingira yetu kwa kiasi kikubwa yanahitaji uthubutu wa kila mmoja wetu kuyahifadhi ili kukabiliana na changamoto za Mbalimali zinazotokana na uharibifu wa Mazingira.akitolea mfano Mvua tukizihitzji haziji kwa wakati,au Kunyesha kupita kiwango jambo ambalo husababisha mafuriko na hivyo kuleta maafa kwa binadam.

TEMEKE BILA UCHAFU INAWEZEKANA.

MKUU WA WILAYA YA TEMEKE APOKEA MAPIPA ZAIDI YA 241 KWA AJILI YA KAMPENI YA “TEMEKE BILA UCHAFU INAWEZEKANA” Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mh F...