Tafuta katika Blogu Hii

Jumamosi, 1 Oktoba 2016

Makamu wa Rais ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan amezindua rasmi Kampeni ya Mti wangu.
Uzinduzi huo umefanyika katika Barabara ya Kilwa wilayani Temeke.
Katika uzinduzi huo Makamu wa Rais amesema kila mmoja wetu ana jukumu la kupanda miti na kuitunza ili kuweza kuhifadhi mazingira pamoja na kukabiliana na mabadilko ya tabia ya nchi pamoja na mabadiliko ya hali ya hewa kwa ujumla.
Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan akizungumza na wananchi kaika  Uzinduzi Kampeni ya Mti wangu uliofanyika katika Barabara Kilwa Temeke. 
 Ameongeza kwa kusema kuwa Mazingira yetu kwa kiasi kikubwa yanahitaji uthubutu wa kila mmoja wetu kuyahifadhi ili kukabiliana na changamoto za Mbalimali zinazotokana na uharibifu wa Mazingira.akitolea mfano Mvua tukizihitzji haziji kwa wakati,au Kunyesha kupita kiwango jambo ambalo husababisha mafuriko na hivyo kuleta maafa kwa binadam.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

TEMEKE BILA UCHAFU INAWEZEKANA.

MKUU WA WILAYA YA TEMEKE APOKEA MAPIPA ZAIDI YA 241 KWA AJILI YA KAMPENI YA “TEMEKE BILA UCHAFU INAWEZEKANA” Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mh F...