Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke Nassib Mbaga amekifunga kituo cha mabasi yaendayo maeneo ya Jaribu,Ikwilili,Rufiji na maeneo mengine ya mkoa pwani kutokana na mmiliki kutokulipa kodi serikalini kwa miaka tisa.
Mkurugenzi amesema amefunga kituo hicho kutokana na mmiliki wake kwenda kinyume cha taratibu za mmiliki wa biashara pia mmiliki huyo alikuwa akiendesha biashara hiyo bila kuwa na hati halali ya biashara jambo lililosababisha akwepe kulipa kodi ya serikali.Mkurugenzi amesema eneo hilo linatambulika kuwa ni kiwanda namba 19 lakini mmiliki huyo amegeuza kituo cha mabasi ya abiria na eneo la biashara.Mkurugenzi amewaomba Madereva watumie kituo cha Mbagala Rangi Tatu wakati taratibu nyingine za kiofisi zinafanyika kutafuta eneo kubwa kwa ajili ya kituo cha daladala katika wilaya hii.
NASSIB MMBAGA.
MKURUGENZI MANISPAA YA TEMEKE.
Mkurugenzi aliongeza kuwa mmiliki eneo hili amekuwa akiingiza sh.milioni 100 kama kodi,lakini serikali haipati hata shilingi moja kutoka kwa mmiliki huyo.
Mkurugenzi amewaomba radhi wananchi waliokuwa wanatumia kituo hicho kwa usumbufu utakaojitokeza na pia amewaomba wawe wavumilivu wakati huu Manispaa inapolitafutia ufumbuzi kituo hicho.
Tafuta katika Blogu Hii
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
TEMEKE BILA UCHAFU INAWEZEKANA.
MKUU WA WILAYA YA TEMEKE APOKEA MAPIPA ZAIDI YA 241 KWA AJILI YA KAMPENI YA “TEMEKE BILA UCHAFU INAWEZEKANA” Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mh F...
-
Shule ya Sekondari Kisarawe ii ni moja kati ya shule zinazopatikana katika wilaya Mpya ya Kigamboni. Shule hii ilianzishwa mwaka 2006 ikiwa...
-
TEMEKE YAKABIDHIWA MABENCHI KUTOKA GOODONE Halmashauri ya Manispaa ya Temeke yakabidhiwa mabenchi kutoka kampuni ya ...
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni