Mkuu wa Wilaya ya Temeke Felix Lyaniva kufanya oparesheni maalum kwa wadaiwa sugu.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam DC Lyaniva ameeleza kuwa zoezi hilo litalenga kukusanya kodi kwa wale wadaiwa sugu ambao wamekuwa wakidaiwa na Halmashauri hiyo kwa muda mrefu.
DC Lyaniva ametaja idadi ya wadaiwa sugu kuwa ni 142 ambapo wadaiwa wa leseni za biashara wakiongoza kwa idadi kubwa ya wadaiwa 69, ushuru wa huduma 52 na wadaiwa sugu kwa upande wa masoko wakiwa ni 21.
Jambo ambalo limepelekea halimashauri hiyo ya wilaya ya Temeke kutofikia malengo ya makusanyo ya kodi ya shilingi bilioni 29 ambapo wamefanikiwa kukusanya bilioni 23 pekee huku zaidi ya bilioni 6 zikibakia kwa wadaiwa sugu.
DC Lyaniva amesisitiza kuwa kwa wasiolipa kabla ya tarehe mosi ya mwezi Julai mwaka huu watachukuliwa hatua kali za kisheria, hivyo ni vyema wakatimiza wajibu huo haraka iwezekanavyo na kufafanua kuwa kwa umuhimu wa jambo hilo ofisi zitakuwa wazi mpaka siku ya jumapili.
Mkuu wa wilaya ya Temeke Felix Lyaniva