Tafuta katika Blogu Hii

Jumamosi, 24 Juni 2017

Mkuu wa wilaya ya Temeke Bw.Felix Lyaniva amesheriki katika zoezi la ufanyaji usafi pamoja na wanachi wa kata ya Buza mtaa wa Mashine ya maji.
Mkuu huyo wa wilaya pia aliweza kuzungumza na wananchi wa kata ya buza katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya CCM kata ya Buza.
katika mazungumzo yake mkuu wa wilaya amewasisitiza wananchi kupenda kufanya usafi katika maeneo yao na sio kusubirri serikali ije kuwafanyia Pia mkuu wa wilaya amewahimiza wananchi wa Buza kushirikiana vyema na jeshi la polisi katika swala zima la ulinzi na usalama wa mitaa yote ya kata ya buza.
Nae mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke Bw.Nassib Mbaga aliwahimiza vijana kupenda kufanya kazi na sio kukaa vijiweni pia aliahidi kudhamini mafunzo ya ujasiriamali kwa vikundi vya vijana ili waweze kujiajili wenyewe.
 Mkuu wa wlaya ya Temeke Felix Lyaniva akishiriki katika usafi kwa kukata nyasi.zoezi hili limefanyika katika kata ya Buza Mtaa wa Mashine ya maji.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

TEMEKE BILA UCHAFU INAWEZEKANA.

MKUU WA WILAYA YA TEMEKE APOKEA MAPIPA ZAIDI YA 241 KWA AJILI YA KAMPENI YA “TEMEKE BILA UCHAFU INAWEZEKANA” Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mh F...