BREAKING
NEWS
MANJI
APOTEZA UDIWANI
Mstahiki Meya wa
Halmashauri ya manispaa ya Temeke Mhe; Abdallah Chaurembo amvua udiwani Mhe;
Yusufali Mehbub Manji ambaye alikua
diwani wa kata ya Mbagala Kuu.
Utenguzi huo ulifatia
uvunjwaji wa kanuni za Halmashauri ya Manispaa ya Temeke za Mwaka 2015 kifungu
cha 72(C) ambacho kinamtaka Diwani pamoja na majukumu mengine aliyonayo lazima
ahudhurie mikutano ya Halmashauri na kamati ndogo ambayo yeye ni mjumbe bila
kukosa.
Aidha sheria ya serikali za Mitaa sura ya
8 ya 1982 kifungu cha 25(5) (a) (b)
kinaeleza kuwa mjumbe wa Baraza la Madiwani ambaye hakuhudhuria vikao vitatu
mfulULIZOzo bila taarifa yeyote ya maandishi kwa Mwenyekiti atakuwa amejiondoa
katika nafasi hiyo. Lakini pia kanuni za
kudumu za Halmashauri ya Manispaa ya Temeke za mwaka 2015 zinaeleza wazi kuwa
kiti cha mjumbe wa Halmashauri kitakuwa wazi endapo mjumbe bila sababu ya
kuridhisha au bila idhini au kibali cha maandishi cha Mwenyekiti, atakosa
kuhudhuria mikutano mitatu (3) ya kawaida ya Halmashauri inayofuatana au kamati
ambayo yeye ni mjumbe, nafasi yake inatakiwa kuwa wazi (kifungu cha 73(1) (m).
Kutokana na vifungu
hivyo vya kanuni vinamlazimu Mstahiki Meya kuengua nafasi hiyo ya Diwani wa
kata ya Mbagala Kuu. Pia mstahiki Meya amemwandikia barua yenye viambatanishi
ya utenguzi huo kama sehemu ya utaratibu unaojulikana katika Ofisi ya Waziri wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali
za Mitaa (TAMISEMI) Mhe; George Simbachawene kuwa nafasi hiyo sasa ipo wazi,
ili taratibu zingine zifuate.
Awali Tarehe
20/2/2017 Mhe; Yusufali Mehbub Manji aliandika barua kwa Mkurugenzi yenye
Kumb.Na. YM-MBGKUU/51/2017 akitoa taarifa ya kutoweza kuhudhuria vikao vya
Halmashauri kutokana na sababu za kiafya bila ya kuwasilisha uthibitisho wa
daktali. Vikao alivyo vikosa baada ya kuandika barua yake ni vile vya tarehe
3-4/3/2017, 18-19/5/2017 na 24-25/8/2017.
Tarehe 22/3/2017
Mkurugenzi alimwandikia barua yenye Kumb. Na TMC/MD/K.11/58/57 akimtaka
awasilishe taarifa za kidaktari kuthibitisha matatizo ya kiafya kama
alivyoeleza kwenye barua yake jambo ambalo hakulitekeleza. Aidha tarehe 22/5/2017
aliandika barua yenye kumb na.
YM/MBGKUU/64/2017 ambayo ilinakilishwa kwa Mkurugenzi akieleza kutohudhuria
vikao vya Halmashauri kwa sababu za kiafya bila kuweka uthibitisho wowote
lakini pia akiweka wazi nia yake ya kutaka kujiuzulu kama hali yake ya afya
haitaimarika.
Mstahiki Meya, Mhe; Abdallah Chaurembo
”kwa kuwa Mhe.
Yusufali Mehbub Manji hakuhudhuria vikao na mikutano ya Halmashauri
inayofuatana bila kutoa taarifa (mikutano ya tarehe
3/2/2016,24/3/2016,1/6/2016,25/8/2016, 24/11/2016, 14-15/2/2017) na vikao vya
kamati ambavyo yeye alikua mjumbe vya tarehe 18/3/2016, 17/8/2016, 8/11/2016,
2/2/2017,(hata vikao na mikutano aliyo toa taarifa alishindwa kuthibitisha
taarifa za ugonjwa) pia amevunja kanuni za Halmashauri pamoja na sheria ya
Serikali za Mitaa sura ya 8 ya mwaka 1982 kifungu 25(5) (a) (b) kama
kinavyosomeka hapo juu, hivyo nawasilisha taarifa rasmi kuwa Bwana Yusufali
Mehbub Manji amekosa sifa ya kuendelea kuwa Diwani wa kata ya Mbagala na kwamba
kata hii itangazwe kuwa iko wazi". alisema Mstahiki Meya wa Halmashauri ya
Manispaa ya Temeke Mhe; Abdallah Chaurembo.