Tafuta katika Blogu Hii

Jumatano, 6 Septemba 2017

BREAKING NEWS
                                 MANJI APOTEZA UDIWANI
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya manispaa ya Temeke Mhe; Abdallah Chaurembo amvua udiwani Mhe; Yusufali Mehbub Manji  ambaye alikua diwani wa kata ya Mbagala Kuu.
Utenguzi huo ulifatia uvunjwaji wa kanuni za Halmashauri ya Manispaa ya Temeke za Mwaka 2015 kifungu cha 72(C) ambacho kinamtaka Diwani pamoja na majukumu mengine aliyonayo lazima ahudhurie mikutano ya Halmashauri na kamati ndogo ambayo yeye ni mjumbe bila kukosa.

 Aidha sheria ya serikali za Mitaa sura ya 8  ya 1982 kifungu cha 25(5) (a) (b) kinaeleza kuwa mjumbe wa Baraza la Madiwani ambaye hakuhudhuria vikao vitatu mfulULIZOzo bila taarifa yeyote ya maandishi kwa Mwenyekiti atakuwa amejiondoa katika nafasi hiyo.  Lakini pia kanuni za kudumu za Halmashauri ya Manispaa ya Temeke za mwaka 2015 zinaeleza wazi kuwa kiti cha mjumbe wa Halmashauri kitakuwa wazi endapo mjumbe bila sababu ya kuridhisha au bila idhini au kibali cha maandishi cha Mwenyekiti, atakosa kuhudhuria mikutano mitatu (3) ya kawaida ya Halmashauri inayofuatana au kamati ambayo yeye ni mjumbe, nafasi yake inatakiwa kuwa wazi (kifungu cha 73(1) (m).

Kutokana na vifungu hivyo vya kanuni vinamlazimu Mstahiki Meya kuengua nafasi hiyo ya Diwani wa kata ya Mbagala Kuu. Pia mstahiki Meya amemwandikia barua yenye viambatanishi ya utenguzi huo kama sehemu ya utaratibu unaojulikana  katika Ofisi ya Waziri wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe; George Simbachawene kuwa nafasi hiyo sasa ipo wazi, ili taratibu zingine zifuate.
Awali Tarehe 20/2/2017 Mhe; Yusufali Mehbub Manji aliandika barua kwa Mkurugenzi yenye Kumb.Na. YM-MBGKUU/51/2017 akitoa taarifa ya kutoweza kuhudhuria vikao vya Halmashauri kutokana na sababu za kiafya bila ya kuwasilisha uthibitisho wa daktali. Vikao alivyo vikosa baada ya kuandika barua yake ni vile vya tarehe 3-4/3/2017, 18-19/5/2017 na 24-25/8/2017. 

Tarehe 22/3/2017 Mkurugenzi alimwandikia barua yenye Kumb. Na TMC/MD/K.11/58/57 akimtaka awasilishe taarifa za kidaktari kuthibitisha matatizo ya kiafya kama alivyoeleza kwenye barua yake jambo ambalo hakulitekeleza. Aidha tarehe 22/5/2017 aliandika barua  yenye kumb na. YM/MBGKUU/64/2017 ambayo ilinakilishwa kwa Mkurugenzi akieleza kutohudhuria vikao vya Halmashauri kwa sababu za kiafya bila kuweka uthibitisho wowote lakini pia akiweka wazi nia yake ya kutaka kujiuzulu kama hali yake ya afya haitaimarika.



                                    
                                     Mstahiki Meya, Mhe; Abdallah Chaurembo 

”kwa kuwa Mhe. Yusufali Mehbub Manji hakuhudhuria vikao na mikutano ya Halmashauri inayofuatana bila kutoa taarifa (mikutano ya tarehe 3/2/2016,24/3/2016,1/6/2016,25/8/2016, 24/11/2016, 14-15/2/2017) na vikao vya kamati ambavyo yeye alikua mjumbe vya tarehe 18/3/2016, 17/8/2016, 8/11/2016, 2/2/2017,(hata vikao na mikutano aliyo toa taarifa alishindwa kuthibitisha taarifa za ugonjwa) pia amevunja kanuni za Halmashauri pamoja na sheria ya Serikali za Mitaa sura ya 8 ya mwaka 1982 kifungu 25(5) (a) (b) kama kinavyosomeka hapo juu, hivyo nawasilisha taarifa rasmi kuwa Bwana Yusufali Mehbub Manji amekosa sifa ya kuendelea kuwa Diwani wa kata ya Mbagala na kwamba kata hii itangazwe kuwa iko wazi". alisema Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke Mhe; Abdallah Chaurembo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

TEMEKE BILA UCHAFU INAWEZEKANA.

MKUU WA WILAYA YA TEMEKE APOKEA MAPIPA ZAIDI YA 241 KWA AJILI YA KAMPENI YA “TEMEKE BILA UCHAFU INAWEZEKANA” Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mh F...