Tafuta katika Blogu Hii

Alhamisi, 22 Februari 2018


TEMEKE YAJENGA WODI YA MAMA NA MTOTO MAJIMATITU

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mhe: Paul Makonda akiambatana na mkuu wa wilaya Felix Lyaniva Pamoja na Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke Nassib Mmbaga, wakipata maelezo kutoka kwa msimamizi wa ujenzi wa wodi ya mama na mtoto katika Zahanati ya Maji matitu. 


Ujenzi ukiendelea katika Zahanati ya Majimatitu


Halmashauri ya Temeke imeanza ujenzi mkubwa wa majengo ya wodi ya Kinamama na mtoto, chumba cha upasuaji, pamoja na chumba cha maabara katika eneo la zahanati ya Majimatitu.



  Ujenzi huo umelenga kuboresha na kutoa huduma bora za Afya lengo likiwa ni kupunguza vifo vya mama na mtoto. Aidha ujenzi huo unatarajiwa kumalizika kabla ya mwezi Mei mwaka huu.

Jumatatu, 5 Februari 2018

MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA MANISPAA YA TEMEKE APOKEA TANI TANO ZA CEMENT



Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa  ya Temeke Ndugu Nassib Mmbaga akabidhiwa Tani tano za cement kutoka Umoja wa Madereva wa Magari yaendayo KUSINI mwa Tanzania(UMAKUTA),akipokea tani hizo Ndugu Mmbaga alisema''Nawashukuru sna viongozi wa UMAKUTA kwa mchango wa cement kwa ajili ya ujenzi wa madarasa,kwakweli mmeonesha moyo wa dhati wa kuunga mkono jitihada za serikali katika maendeleo ya sekta ya elimu katika halmashauri yetu.'' 



Ndugu Mmbaga aliongeza kwa kutoa Takwimu za usajili wa wanafunzi tangu mwezi January mpaka sasa imefikia elfu thelathini ikijumuisha na shule za watu binafsi.Pia alisema bado tuna upungufu wa idadi wa vyumba vya madarasa ya sekondari 130.Ambayo yanaendelea kujengwa mpaka sasa ni madarasa 90.




Hapohapo alimshukuru Bw.Martin Lumbanga ambae amejitolea heka nne kwa ajili ya ujenzi wa shule.Hata hivyo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Temeke ametoa wito kwa wadu wengine kujitokeza kwa wingi ili kuchangia maendeleo mbalimbali ya Temeke.
Akongea kwa niaba ya umoja wa UMAKATA katibu wa madereva Bw.Yusuph Ismail aliwataka wadau wengine wajitokeze hata kama wana uwezo kidogo ili kusaidia kukamilisha ujenzi wa madarasa.







Pia Afsa elimu vifaa na takwimu Bi.Veronica Jinga Lyanga aliwashukuru UMAKUTA na kusema '' tumekua na uhaba wa vyumba vya madarasa pamoja na tatizo la wanafunzi kuingia kwa zamu mashuleni,lakini kwa kupitia msaada huu tutaweza kulimaliza tatizo hili linalotukabili.Nitoe wito kwa wadau wengine kujitokeza.





TEMEKE BILA UCHAFU INAWEZEKANA.

MKUU WA WILAYA YA TEMEKE APOKEA MAPIPA ZAIDI YA 241 KWA AJILI YA KAMPENI YA “TEMEKE BILA UCHAFU INAWEZEKANA” Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mh F...