Mkurugenzi wa Halmashauri ya
Manispaa ya Temeke Ndugu Nassib Mmbaga
akabidhiwa Tani tano za cement kutoka Umoja wa Madereva wa Magari yaendayo
KUSINI mwa Tanzania(UMAKUTA),akipokea tani hizo Ndugu Mmbaga alisema''Nawashukuru sna
viongozi wa UMAKUTA kwa mchango wa cement kwa ajili ya ujenzi wa
madarasa,kwakweli mmeonesha moyo wa dhati wa kuunga mkono jitihada za serikali
katika maendeleo ya sekta ya elimu katika halmashauri yetu.''
Ndugu Mmbaga
aliongeza kwa kutoa Takwimu za usajili wa wanafunzi tangu mwezi January mpaka
sasa imefikia elfu thelathini ikijumuisha na shule za watu binafsi.Pia alisema
bado tuna upungufu wa idadi wa vyumba vya madarasa ya sekondari 130.Ambayo
yanaendelea kujengwa mpaka sasa ni madarasa 90.
Hapohapo alimshukuru Bw.Martin
Lumbanga ambae amejitolea heka nne kwa ajili ya ujenzi wa shule.Hata hivyo
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Temeke ametoa wito kwa wadu wengine kujitokeza kwa
wingi ili kuchangia maendeleo mbalimbali ya Temeke.
Akongea kwa niaba ya umoja wa
UMAKATA katibu wa madereva Bw.Yusuph Ismail aliwataka wadau wengine wajitokeze
hata kama wana uwezo kidogo ili kusaidia kukamilisha ujenzi wa madarasa.
Pia Afsa elimu vifaa na takwimu
Bi.Veronica Jinga Lyanga aliwashukuru UMAKUTA na kusema '' tumekua na uhaba wa
vyumba vya madarasa pamoja na tatizo la wanafunzi kuingia kwa zamu
mashuleni,lakini kwa kupitia msaada huu tutaweza kulimaliza tatizo hili
linalotukabili.Nitoe wito kwa wadau wengine kujitokeza.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni