Tafuta katika Blogu Hii

Jumatatu, 30 Julai 2018

DC Temeke ahamasisha wananchi kuwa na vitambulisho vya Taifa


Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mhe:Felix Lyaniva akutana na wananchi wenye uhitaji wa kitambulisho cha Taifa na kuwahimiza umuhimu wa kuhakikisha wanasajiliwa ili kupatiwa huduma hiyo.

Akizungumza na wananchi hao katika ofisi za NIDA kanda ya Temeke,Mhe:Lyaniva aliwashauri wananchi hao kuhakikisha wanajisajili ili kupatiwa huduma hiyo ambayo itawawezesha kutambulika kisheria.

“NIDA inatoa huduma ya kitambulisho kwa mwananchi yoyote ilimradi awe ametimiza taratibu zote za viambata vinavyotakiwa”alisema.



 Mhe:Lyaniva alisema anatambua changamoto ya rasilimali watu inayowakabili katika kupatiwa huduma hiyo na kuahidi kulifanyia kazi kwa wakati ili kuokoa muda na kuhakikisha kila mwananchi wa Manispaa ya Temeke anapatiwa kitambuisho hicho.

Pamoja na hayo aliwataka watumishi wa NIDA kuwa waadilifu na waaminifu katika kutimiza majukumu yao ya kila siku.
Nae mratibu wa NIDA kanda ya Temeke ndug:Paul Marwa alisema ili kupatiwa kitambuisho cha taifa inapaswa kuambatanisha na viambata vitatu kati ya vifuatavyo,cheti cha kuzaliwa, cheti cha elimu ya msingi, pasiya kusafiria, cheti cha elimu ya sekondari,leseni ya udereva, kadi ya bima ya afya, kadi ya mpiga kura,pamoja na nambari ya mlipa kodi (Tin namba).

TEMEKE BILA UCHAFU INAWEZEKANA.

MKUU WA WILAYA YA TEMEKE APOKEA MAPIPA ZAIDI YA 241 KWA AJILI YA KAMPENI YA “TEMEKE BILA UCHAFU INAWEZEKANA” Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mh F...