Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mhe:Felix Lyaniva
akutana na wananchi wenye uhitaji wa kitambulisho cha Taifa na kuwahimiza
umuhimu wa kuhakikisha wanasajiliwa ili kupatiwa huduma hiyo.
Akizungumza na wananchi hao katika ofisi za NIDA
kanda ya Temeke,Mhe:Lyaniva aliwashauri wananchi hao kuhakikisha wanajisajili
ili kupatiwa huduma hiyo ambayo itawawezesha kutambulika kisheria.
“NIDA inatoa huduma ya kitambulisho kwa mwananchi
yoyote ilimradi awe ametimiza taratibu zote za viambata vinavyotakiwa”alisema.
Mhe:Lyaniva
alisema anatambua changamoto ya rasilimali watu inayowakabili katika kupatiwa
huduma hiyo na kuahidi kulifanyia kazi kwa wakati ili kuokoa muda na
kuhakikisha kila mwananchi wa Manispaa ya Temeke anapatiwa kitambuisho hicho.
Pamoja na hayo aliwataka watumishi wa NIDA kuwa
waadilifu na waaminifu katika kutimiza majukumu yao ya kila siku.
Nae mratibu wa NIDA kanda ya Temeke ndug:Paul
Marwa alisema ili kupatiwa kitambuisho cha taifa inapaswa kuambatanisha na
viambata vitatu kati ya vifuatavyo,cheti cha kuzaliwa, cheti cha elimu ya
msingi, pasiya kusafiria, cheti cha elimu ya sekondari,leseni ya udereva, kadi
ya bima ya afya, kadi ya mpiga kura,pamoja na nambari ya mlipa kodi (Tin namba).
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni