Tafuta katika Blogu Hii

Alhamisi, 6 Desemba 2018

Halmashauri ya Manispaa Manispaa ya Temeke kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar -Es- Salaam na wizara ya afya,Maendeleo ya Jamii jinsia wazee na watoto inategemea kufanya kampeni maalum ya utoaji wa dawa za kingatiba kwa Magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele. Miongoni mwa magonjwa hayo yamo ndani ya jamii maskini.Magonjwa hayo ni Ukoma, Matende na Mabusha(Ngirimaji), Minyoo ya Tumbo, Usubi, Homa ya dengu, Homa ya malale na Homa ya Ini.
Akizungumza katika uzinduzi huo Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mh.Felix Lyaniva alihimiza wajumbe wa kamati kwenda kuhamasisha vizuri kwa wananchi ili wajitokeze kwa ajili ya kupata dawa za kinga tiba ya magonjwa yasiyopewa kipaumbele,ambapo zoezi hilo la ugawaji dawa litadumu kwa muda wa siku 6 kuanzia tarehe 15/12/2018 mpaka tarehe 20 /12/2018 wanaotakiwa kupata dawa hizo ni wenye umri kuanzia miaka 5 na kuendelea.Dawa hizo zitagawiwa katika maeneo tofauti tofauti ikiwemo kwenye vituo vya Afya, Mashuleni,kwenye makazi ya watu ,Baadhi ya ofisi za serikali za Mitaa n.k, walengwa ni wananchi wote wa Temeke wapatao 1,136,057 ambao ni asilimia 80% ya wakazi wote kati ya 1,420,071 kulingana na takwimu ya sensa ya 2012.
vituo vya kutolea dawa hizo vipo 161(110 vya kudumu na 51 vya kuhamahama kwa muda wa siku zote sita.
Nae Mganga mkuu wa Manispaa ya Temeke Ndg.Gwamaka Mwabulambo aliomba wakazi wa Temeke kuja kupata dawa hizo ifikapo tarehe 15 mwezi huu na dawa hizo zitatolewa bure bila gharama yoyote na hazina madhara yoyote
Hivyo wananchi mnaombwa kujitokeza kupata dawa ya kinga tiba za magonjwa yasiyopewa kipaumbele.

Mh.Felix Lyaniva akipata dawa za kinga ya magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

TEMEKE BILA UCHAFU INAWEZEKANA.

MKUU WA WILAYA YA TEMEKE APOKEA MAPIPA ZAIDI YA 241 KWA AJILI YA KAMPENI YA “TEMEKE BILA UCHAFU INAWEZEKANA” Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mh F...