Wadau
wa malezi ya watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi (JSI) wametoa mafunzo
ya mfumo jumuishi kwawatendaji na wakuu wa idara na vitengo wa Halmashauri ya
Manispaa ya Temeke.Mfumo huo umewekwa na serikali kwa kushirikiana na wadau
kama WAMATA na(JSI) ili kutoa huduma kwa pamoja kwa watoto wanaoishi katika
mazingira hatarishi pamoja na watu wanaoishi na virusi vya ukimwi na sio kila mdau kwenda au kupeleka huduma
kipekee
Afisa wa maendeleo ya jamii kutoka wizara ya Afya Bi Asia Jingu akitoa mafunzo kwa wakuu wa idara na watendaji wa kata wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke.
Akitoa mafunzo hayo Bi Asia Jingu amesema mfumo huu ni
muhimu kwani utawezesha kuweka taratibu za utoaji wa huduma kwa watoto
wanaoishi katika mazingira hatarishi na si kila taasisi ama mdau kuwa na
utaratibu wake jambo ambalo lilikuwa likisababisha baadhi ya watoto kukosa
huduma kutokana na sababu mablimbali.pia Mfumo huu utahamasisha ushirikiano wa
karibu kati ya wadau na taasisi
zinazojihusisha na kuhudumia watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi.
Bi Asia Jingu pia amesema watoa huduma kwa watoto wanaoishi
katika mazingira magumu wanatakiwa kutoa huduma kwa uweledi mkubwa kwani kazi
hii ni ya kujitolea,kwa hiyo kwa wale wote watakaopata mafunzo kwa ajili ya
huduma hiyo katika Mitaa mbalimbali wawe waadilifu kwa watoto na pia kutoa
huduma bila ubaguzi kwa watoto wala kutowadhuru watoto hao walio katika
mazingira magumu.