Mkuu wa wilaya ya Temeke Bw Felix Lyaniva amefanya kikao na
wenyeviti wa serikali za mitaa yote ya Halmashauri ya Manispaa ya Temeke lengo
likiwa kujadili hali ya ulinzi na usalama katika Manispaa ya Temeke.
Akizungumza na wenyeviti hao Mkuu wa wilaya amewasisitiza
wenyeviti hao kuhakikisha wanaunda vikundi vya ulinzi shirikishi katika Mitaa
yao ili kuimarisha ulinzi katika Mitaa na pia kuwahimiza wananchi kutoa taarifa
polisi pindi wanapoona dalili za uharifu,ama kugundua kundi lauharifu kwani kwa
kufanya hivyo tayari kutasaidia kudumisha ulinzi katika eneo husika.
Mkuu wa wilaya ya Temeke Bw Felix Lyaniva akizungumza na wenyeviti wa serikali za Mitaa hawapo pichani.
Pia Mkuu wa wilaya aliwasisitiza wenyeviti kusimamia wazazi
wenye watoto walio na umri wa kwenda shule kuhakikisha wanawapeleka watoto hao
shule na kuhakikisha wanafika shule na si kukaa katika vijiwe kwani huko ndiko
huunda vikundi vya Panya road ambavyo baadae huleta matatizo kwa wananchi.Pia
aliwasisistiza wenyeviti hao kuendelea kulifanyia kazi daftari la makazi ili
kuweza kutambua wageni katika mtaa na pia kutoa taarifa kwa mamlaka husika
pindi wanapokuwa na mashaka na watu wapya
wanaohamia katika Mitaa yao.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni