Tafuta katika Blogu Hii

Alhamisi, 6 Aprili 2017

WADAU WA MALEZI YA WATOTO WASHIO KATKA MAZINGIRA MAGUMU WATOA MAFUNZO.

Wadau wa malezi ya watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi (JSI) wametoa mafunzo ya mfumo jumuishi kwawatendaji na wakuu wa idara na vitengo wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke.Mfumo huo umewekwa na serikali kwa kushirikiana na wadau kama WAMATA na(JSI) ili kutoa huduma kwa pamoja kwa watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi pamoja na watu wanaoishi na virusi vya ukimwi  na sio kila mdau kwenda au kupeleka huduma kipekee




















 Afisa wa maendeleo ya jamii kutoka wizara ya Afya Bi Asia Jingu akitoa mafunzo kwa wakuu wa idara na watendaji wa kata wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke.

Akitoa mafunzo hayo Bi Asia Jingu amesema mfumo huu ni muhimu kwani utawezesha kuweka taratibu za utoaji wa huduma kwa watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi na si kila taasisi ama mdau kuwa na utaratibu wake jambo ambalo lilikuwa likisababisha baadhi ya watoto kukosa huduma kutokana na sababu mablimbali.pia Mfumo huu utahamasisha ushirikiano wa karibu kati ya wadau na  taasisi zinazojihusisha na kuhudumia watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi.
Bi Asia Jingu pia amesema watoa huduma kwa watoto wanaoishi katika mazingira magumu wanatakiwa kutoa huduma kwa uweledi mkubwa kwani kazi hii ni ya kujitolea,kwa hiyo kwa wale wote watakaopata mafunzo kwa ajili ya huduma hiyo katika Mitaa mbalimbali wawe waadilifu kwa watoto na pia kutoa huduma bila ubaguzi kwa watoto wala kutowadhuru watoto hao walio katika mazingira magumu.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

TEMEKE BILA UCHAFU INAWEZEKANA.

MKUU WA WILAYA YA TEMEKE APOKEA MAPIPA ZAIDI YA 241 KWA AJILI YA KAMPENI YA “TEMEKE BILA UCHAFU INAWEZEKANA” Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mh F...