HALMASHAURI YA MANISPAA YA TEMEKE YAPATA NAIBU MEYA MPYA
Halmashauri ya Manispaa
ya Temeke imepata Naibu Meya mpya,
katika kikao cha baraza la madiwani ambapo kisheria kila mwaka hupatikana Naibu
Meya mpya. Katika uchaguzi huo kulikua na wagombea wawili Mh:Benjamini Ndalichako
diwani wa kata ya Changombe na Mh:Juma Rajab Mkenga diwani wa kata ya Miburani. Ambapo katika kinyang'anyiro hicho Mh:Juma Rajabu Mkenga aliibuka mshindi kwa kura 18
kati ya kura 29 ya kura zilizopigwa,huku mpinzani wake akiwa na kura 11.
Mara baada ya
kupata ushindi huo Mh:Mkenga aliwashukuru wapiga kura wote na kuwaomba
washirikiane katika kuijenga Temeke mpya.
Pia katika baraza
hilo ulifanyika uchaguzi wa viongozi wa kamati mbalimbali ambazo zitashirikiana
katika mambo ya kijamii na maendeleo ya Temeke, kamati hizo ni pamoja na kamati
ya Uchumi Afya na Elimu Mwenyekiti ni Mhe: Abdallah S Mtinika, Kamati ya MipangoMiji na Mazingira Mwenyekiti ni Mhe: Ramadhan Likimangiza,Kamati ya Fedha na Uongozi Mwenyekiti ni Mhe: Abdallah J Chaurembo, Kamati ya Kudhibiti Ukimwi mwenyekiti ni Mhe Juma R Mkenga.
Imetolewa na ofisi
ya Habari na Uhusiano Temeke.