UKAGUZI WA MIRADI YA WAHESHIMIWA MADIWANI
Madiwani wa wilaya na halmashuri ya Manspaa ya Temeke wakiongozwa
na Naibu Meya Mh; Faisal Salum, watembelea miradi mbalimbali ya Manispaa Temeke
yenye thamani ya zaidi ya Bilioni 22. Ambayo imefikia hatua nzuri zenye
kuridhisha na kukaribia kukamilika kabisa ifikapo mwezi pili 2018. Miradi hiyo
n ile inayosimamiwa na DMDP, Halmashauri ya Temeke na World Bank.
Waheshimiwa wamefurahishwa na kile walichokikuta katika
kuboresha na kuinua miundo mbinu ya Manispaa hiyo. Miradi hiyo ikikamilika
italeta urahisi katika utoaji huduma
katika maeneo hayo.
Moja ya mradi ulio katika hali nzuri ni ule wa usambazaji
maji ambao ukikamilika unatazamiwa kusaidia wakazi wa Mbuyuni, Azimio, Mbagala
kuu na Kizuiani. Miradi mingine ni kama ujenzi wa barabara ya Mwanamtoti,ujenzi
wa barabara ya Kijichi Toangoma wenye urefu wa 3.1KM, ujenzi wa daraja lenye
urefu wa mita 16,Ofisi za Mradi wa DMDP umekamilika kwa zaidi ya asilimia 95%.
Ujenzi wa madarasa kidato cha Tano na Sita shule ya Sekondari Mbagala,
ukarabati wa vyumba 20 vya madarasa shule ya msingi Mbagala Anex, ujenzi wa
vyumba 2 vya madarasa shule ya msingi Karume.
Hata hivyo Mh;Naibu Meya amepinga vikali kasi ndogo ya
wakandarasi ambao wanakwamisha miradi kukamilika kwa wakati kwa kusingizia mvua
na mabadiliko ya hali ya tabia nchi, hivyo amesema hatamvumilia yeyote atakaye
onekana kwenda kinyume na mikataba waliokubaliana. Hata hivyo amewapongeza
wakuu wa Idara, watendaji na watumishi wote ambao wanashiriki kikamilifu katika
zoezi hilo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni