Tafuta katika Blogu Hii

Alhamisi, 24 Agosti 2017

HALMASHAURI YA MANISPAA YA TEMEKE  YAPATA NAIBU MEYA MPYA

Halmashauri ya Manispaa ya Temeke imepata Naibu  Meya mpya, katika kikao cha baraza la madiwani ambapo kisheria kila mwaka hupatikana Naibu Meya mpya. Katika uchaguzi huo kulikua na wagombea wawili Mh:Benjamini Ndalichako diwani wa kata ya Changombe na Mh:Juma Rajab Mkenga diwani wa kata ya  Miburani. Ambapo katika kinyang'anyiro hicho  Mh:Juma Rajabu Mkenga aliibuka mshindi kwa kura 18 kati ya kura 29  ya kura zilizopigwa,huku mpinzani wake akiwa na kura 11.

Mara baada ya kupata ushindi huo Mh:Mkenga aliwashukuru wapiga kura wote na kuwaomba washirikiane katika kuijenga Temeke mpya.
Pia katika baraza hilo ulifanyika uchaguzi wa viongozi wa kamati mbalimbali ambazo zitashirikiana katika mambo ya kijamii na maendeleo ya Temeke, kamati hizo ni pamoja na kamati ya Uchumi Afya na Elimu Mwenyekiti ni Mhe: Abdallah S Mtinika, Kamati ya MipangoMiji na Mazingira Mwenyekiti ni Mhe: Ramadhan Likimangiza,Kamati ya Fedha na Uongozi Mwenyekiti ni Mhe: Abdallah J Chaurembo, Kamati ya Kudhibiti Ukimwi mwenyekiti ni Mhe Juma R Mkenga.


Imetolewa na ofisi ya Habari na Uhusiano Temeke.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

TEMEKE BILA UCHAFU INAWEZEKANA.

MKUU WA WILAYA YA TEMEKE APOKEA MAPIPA ZAIDI YA 241 KWA AJILI YA KAMPENI YA “TEMEKE BILA UCHAFU INAWEZEKANA” Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mh F...