Manispaa ya Temeke yafanya Baraza la
madiwani leo katika ukumbi wa Iddi Nyundo uliopo ndani ya manispaa.Akizungumza
katika baraza la madiwani kuanza Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mh:Felix Lyaniva
alikumbusha watendaji pamoja na madiwani kusimamia sera ya elimu bure katika
kata zao. Aliwataka kuelimisha umma kuwa elimu bure inawezekana kama dhamira ya
serikali ya awamu ya tano ya Dr John Pombe Magufuli inavyokazana kulitekeleza
hilo.
Pia amewaasa wakuu wa shule ambao
wanavunja sheria ya kuchukua tozo yoyote ya kielimu kuacha mara moja. Pia
aliwapongeza madiwani wote kwa namna wanavyotekeleza sheria za utawala bora.Na
aliwataka madiwani kuhakikisha makusanyo ya kodi yanapatikana kulingana na
makadirio ya bajeti ya Halmashauri.Kisha akawatakia kikao kizuri chenye mafanikio.
Mstahiki Meya Abdallah Chaurembo
alimpongeza Mh: Lyaniva,juhudi zake kuhimiza maendeleo na akahaidi kuyafanyia
kazi. Madiwani walipokea taarifa za utekelezaji kazi kutoka katika kata kwa
kipindi cha robo ya pili Oktoba-Disemba,2017. Taarifa hizo zilijadiliwa kwa
kina ikiwemo miradi ya maendeleo inayoendelea katika kata na ile ambayo
imekwisha kukamilika. Hata hivyo baraza lilijadili makusanyo ya kodi katika
kila kata ambapo kata ya Kilungule chini ya diwani Said Fella imeongoza katika
ukusanyaji wa kodi.
Pia makusanyo ya huduma ya uzoaji
taka kata ya Yombo Vituka yalipanda na kufikia kiasi cha sh:36,822,350.00 na
kupongezwa na madiwani.
Hata hivyo Baraza la madiwani
lilidhibitisha mihtasari ya mikutano ya Halmashauri na vikao vya kamati za
kudumu katika robo ya pili kwa kipindi cha Oktoba-Disemba 2017.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke
Ndug:Nasibu Mmbaga aliwakumbusha watendaji kufanya kazi kwa juhudi katika
kuhakikisha wanajikita katika kuboresha na kuwekeza sector ya elimu na afya.
Katika robo ya pili ya bajeti manispaa imeweza kujenga matundu 98 ya
vyoo,madawati 110,000 na madarasa 480 katika shuletofauti.Aitha, shilingi
milioni 400 zimetengwa kwaajili ya marekebisho na ujenzi wa miundo mbinu ya
afya na elimu katika kata za Yombo Vituka na Kata ya Sandari.Pia Mkurugenzi
Mmbaga alisisitiza utumiaji wa force account ili kupunguza gharama katika
utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.Alitoa mfano wa ujenzi wa daraja
la Kibonde maji ambalo limejengwa kwa mfumo huo.
Mstahiki Meya akiahirisha kikao
amewaagiza watendaji wa kata na mitaa kusimamia ukusanyaji wa kodi, ili kuleta
maendeleo ya haraka ndani ya Manispaa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni