Tafuta katika Blogu Hii

Jumatano, 6 Juni 2018

Temeke yazidi kung'aa ujenzi wa vituo vya afya



Temeke ni miongoni mwa Halmashauri za Dar es Salaam ambayo inatekeleza miradi ya ukarabati na ujenzi wa vituo vya afya  kwa kutumia force account. Mradi huo wenye malengo ya kuboresha huduma ya afya mama na mtoto ili kupunguza vifo.



Timu kutoka OR TAMISEMI na Mkoa ilifanya ukaguzi wa ujenzi wa miradi hiyo ili kujiridhisha na ubora wa ujenzi huo.
Kutoka TAMISEMI timu ili ongozwa  na katibu wa afya OR TAMISEMI Ndg:Deogratius Maufi, ilifanya ukaguzi kituo cha afya Yombo vituka na Zahanati ya Majimatitu ambapo iliridhishwa na kasi inayoendelea katika ujenzi wa majengo hayo kulingana na muda uliopangwa. Pamoja na ukaguzi wa matumizi sahihi ya pea za miradi hiyo.Vilevile ilitoa mapendekezo juu ya ukamilishwa wa ujenzi huo.



''ujenzi unaridhisha,pia inaendana na muda ambao ulipangwa kumalizika.Ambapo  awali ilikua yakamilike may 31,lakini kufikia mwezi wa saba tunaamini yatakua yanatumiwa kwaajili ya utoaji huduma. kwani Serikali imeshaanza kutoa vifaa vitavyohitajika katika upanuzi wa vituo hivyo vya afya ikiwemo watumishi na vifaa tiba ili kufikia hatua za mwisho za ukamilikaji''. Alisema Maufi.





Hata hivyo Maufi aliongeza kuendelea kuboresha mapungufu machache yanayorekebishika ili mradi kufikia mwisho.
Manispaa ya temeke ilipokea jumla ya fedha 800,000,000/= toka Ofisi ya Rais-TAMISEMI kwa ajili ya ukarabati wa kituo cha Afya Yombo Vituka pamoja na Zahanati ya Majimatitu ili viweze kutoa huduma bora kwa wananchi hususani huduma za upasuaji wa dharura kwa mama wajawazito  walioshindwa kujifungua kwa njia ya kawaida ili kupunguza vifo vya mama wajawazito pamoja na watoto wachanga.



Ujenzi wa vituo vya afya Yombo Vituka na Majimatitu unajumuisha jengo la upasuaji, wodi ya akina mama na mtoto pamoja na nyumba ya mtumishi.
Vituo hivyo vyote vimefikia hatua nzuri ili kuweza kukamilika kwake.

Ijumaa, 1 Juni 2018

Temeke kuzidi kung'aa kupitia miradi ya DMDP

Wananchi Temeke wahimizwa kupanda Miti ya Matunda


Wilaya ya Temeke yafanya uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya Mazingira Duniani kiwilaya.
Akizungumza na wanachi katika sherehe hizo Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mh:Felix Lyaniva alisema “Jiji letu limepwa heshima kubwa ya kuwa mwenyeji wa sherehe za kilele kitaifa, na kwa ngazi ya kiwilaya tumeanza leo kwa kupanda miti na kufanya usafi katika maeneo yote ya Hospitali.Hii ni kutokana na changamoto kubwa ya mazingira inayojitokeza mara kwa mara”.



Alisema maadhimisho haya yatafanyika Mkoa wa Dar es Salaam katika viwanja vya Mnazi Mmoja na kauli mbiu “Mkaa ni gharama, Tumia nishati mbadala”Alisisitiza.
Aliongeza kuwa maadhimisho hayo yatatanguliwa na shughuli mbalimbali za uhamasishaji juu ya utunzaji na uhifadhi wa mazingira.
Miongini mwa shughuli hizo ni makongamano yatakayohusisha wadau mbalimbali wa mazingira,maonesho ya shughuli za mazingira,upandaji miti na kampeni za usafi katika maeneo mbalimbali.
 Lyaniva alisisitiza kuwa shughuli hizi zitafanyika kwa wiki nzima kuanzia tarehe 31 Juni mpaka tarehe 5 Juni ambapo itakuwa siku ya kilele.
Vile vile alibainisha kuwa ukataji wa miti kwa matumizi mbalimbali ikiwemo nishati huleta athari za kimazingira,kama vile ongezeko la hewa ya ukaa na joto duniani,kuyeyuka kwa barafu katika vilele vya milima,kuongeeka kwa kina cha habari,ukame na mafuriko.



Aidha ili kutekeleza jitihada za kupunguza matumizi ya nishati itokanayo na miti Mkoa wa Dar es Salaam,kupitia mpango wake wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi umefanikiwa kujenga ukuta ili kuzuia mmomonyoko katika kinga ya bahari ya Hindi.
Pamoja na utumiaji wa majiko banifu badala ya mkaa.Lengo kuu likiwa kuhifadhi misitu tuliyonayo nchini.
Wilaya ya Temeke imekuwa ikitekeleza tamko la Mh.Rais John Pombe Magufuli la “usafi kwanza” la tarehe 9 Disemba 2015.
Pamoja na juhudi zinazofanywa,Wilaya ya Temeke imeamua kuweka mazingira safi na yenye kuvutia kwa kupanda miti kupitia kauli mbiu ya “Mti wangu”.




Aidha Wilaya ya Temeke imekuwa na utaratibu wa kufanya usafi kwa kila mwisho wa wiki (Jumamosi) na Jumamosi ya mwisho wa mwezi.

TEMEKE BILA UCHAFU INAWEZEKANA.

MKUU WA WILAYA YA TEMEKE APOKEA MAPIPA ZAIDI YA 241 KWA AJILI YA KAMPENI YA “TEMEKE BILA UCHAFU INAWEZEKANA” Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mh F...