Temeke ni miongoni
mwa Halmashauri za Dar es Salaam ambayo inatekeleza miradi ya ukarabati na
ujenzi wa vituo vya afya kwa kutumia force
account. Mradi huo wenye malengo ya kuboresha huduma ya afya mama na mtoto ili
kupunguza vifo.
Timu kutoka OR TAMISEMI
na Mkoa ilifanya ukaguzi wa ujenzi wa miradi hiyo ili kujiridhisha na ubora wa
ujenzi huo.
Kutoka TAMISEMI
timu ili ongozwa na katibu wa afya OR
TAMISEMI Ndg:Deogratius Maufi, ilifanya ukaguzi kituo cha afya Yombo vituka na
Zahanati ya Majimatitu ambapo iliridhishwa na kasi inayoendelea katika ujenzi
wa majengo hayo kulingana na muda uliopangwa. Pamoja na ukaguzi wa matumizi
sahihi ya pea za miradi hiyo.Vilevile ilitoa mapendekezo juu ya ukamilishwa wa
ujenzi huo.
''ujenzi
unaridhisha,pia inaendana na muda ambao ulipangwa kumalizika.Ambapo awali ilikua yakamilike may 31,lakini kufikia
mwezi wa saba tunaamini yatakua yanatumiwa kwaajili ya utoaji huduma. kwani
Serikali imeshaanza kutoa vifaa vitavyohitajika katika upanuzi wa vituo hivyo
vya afya ikiwemo watumishi na vifaa tiba ili kufikia hatua za mwisho za
ukamilikaji''. Alisema Maufi.
Hata hivyo Maufi
aliongeza kuendelea kuboresha mapungufu machache yanayorekebishika ili mradi
kufikia mwisho.
Manispaa ya temeke
ilipokea jumla ya fedha 800,000,000/= toka Ofisi ya Rais-TAMISEMI kwa ajili ya
ukarabati wa kituo cha Afya Yombo Vituka pamoja na Zahanati ya Majimatitu ili
viweze kutoa huduma bora kwa wananchi hususani huduma za upasuaji wa dharura
kwa mama wajawazito walioshindwa
kujifungua kwa njia ya kawaida ili kupunguza vifo vya mama wajawazito pamoja na
watoto wachanga.
Ujenzi wa vituo vya
afya Yombo Vituka na Majimatitu unajumuisha jengo la upasuaji, wodi ya akina
mama na mtoto pamoja na nyumba ya mtumishi.
Vituo hivyo vyote
vimefikia hatua nzuri ili kuweza kukamilika kwake.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni