Wilaya ya Temeke yafanya uzinduzi wa maadhimisho
ya wiki ya Mazingira Duniani kiwilaya.
Akizungumza na wanachi katika sherehe hizo Mkuu
wa Wilaya ya Temeke Mh:Felix Lyaniva alisema “Jiji letu limepwa heshima kubwa
ya kuwa mwenyeji wa sherehe za kilele kitaifa, na kwa ngazi ya kiwilaya
tumeanza leo kwa kupanda miti na kufanya usafi katika maeneo yote ya Hospitali.Hii
ni kutokana na changamoto kubwa ya mazingira inayojitokeza mara kwa mara”.
Alisema maadhimisho haya yatafanyika Mkoa wa Dar
es Salaam katika viwanja vya Mnazi Mmoja na kauli mbiu “Mkaa ni gharama, Tumia
nishati mbadala”Alisisitiza.
Aliongeza kuwa maadhimisho hayo yatatanguliwa na
shughuli mbalimbali za uhamasishaji juu ya utunzaji na uhifadhi wa mazingira.
Miongini mwa shughuli hizo ni makongamano
yatakayohusisha wadau mbalimbali wa mazingira,maonesho ya shughuli za
mazingira,upandaji miti na kampeni za usafi katika maeneo mbalimbali.
Lyaniva
alisisitiza kuwa shughuli hizi zitafanyika kwa wiki nzima kuanzia tarehe 31
Juni mpaka tarehe 5 Juni ambapo itakuwa siku ya kilele.
Vile vile alibainisha kuwa ukataji wa miti kwa
matumizi mbalimbali ikiwemo nishati huleta athari za kimazingira,kama vile
ongezeko la hewa ya ukaa na joto duniani,kuyeyuka kwa barafu katika vilele vya
milima,kuongeeka kwa kina cha habari,ukame na mafuriko.
Aidha ili kutekeleza jitihada za kupunguza
matumizi ya nishati itokanayo na miti Mkoa wa Dar es Salaam,kupitia mpango wake
wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi umefanikiwa kujenga ukuta ili kuzuia
mmomonyoko katika kinga ya bahari ya Hindi.
Pamoja na utumiaji wa majiko banifu badala ya
mkaa.Lengo kuu likiwa kuhifadhi misitu tuliyonayo nchini.
Wilaya ya Temeke imekuwa ikitekeleza tamko la
Mh.Rais John Pombe Magufuli la “usafi kwanza” la tarehe 9 Disemba 2015.
Pamoja na juhudi zinazofanywa,Wilaya ya Temeke
imeamua kuweka mazingira safi na yenye kuvutia kwa kupanda miti kupitia kauli
mbiu ya “Mti wangu”.
Aidha Wilaya ya Temeke imekuwa na utaratibu wa
kufanya usafi kwa kila mwisho wa wiki (Jumamosi) na Jumamosi ya mwisho wa
mwezi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni