Maafisa afya wote wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke wamehudhuria
mafunzo ya namna ya kujikinga na ugonjwa wa Ebola. Mafunzo hayo yamefanyika
katika ukumbi wa Iddi Nyundo uliopo Manispaa,yaliyoendeshwa na wataalamu kutoka
Ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam wakishirikiana na wataalamu kutoka
Wizara ya Afya.
Mafunzo hayo yenye lengo la kuwajengea uwezo wataalamu wote
wa afya wa Halmashauri ili kukabiliana na ugonjwa huo endapo utatokea.
Mtaalamu kutoka Wizara ya Afya na maendeleo ya jamii kitengo
cha Epidermiology Bib:Vida Mmbaga, ambae alifundisha mambo mbalimbali ikiwemo
jinsi ya kujikinga, kumtambua mgonjwa na namna ya kumuhudumia mgonjwa wa Ebola.Aliwaambia
wataalamu hao ni muhimu kuwa na vikao mbalimbali vya ndani ili kujadili namna
ya kujipanga kutokomeza virusi hivyo, ikiwemo kujiandaa na vifaa na eneo
maalaumu la kumuhudumia mgonjwa mwenye dalili zitokanazo na ugonjwa huo endapo
ugonjwa huo ukitokea. Pia aliwakumbusha maafisa afya kuendelea kujifunza juu ya
kuukabili ugonjwa huo kwa kupata mafunzo ya mara kwa mara.
Hata hivyo mafunzo hayo yataendelea kwa ngazi zote za
Halmashauri mpaka kumfikia mwananchi wa ngazi ya chini anayeishi Temeke.
Ebola ni ugonjwa unaosababishwa na virusi vya homa ya hemoraji
(kumwaga damu kwa sana). Kati ya watuu 10 waliopata virusi vya ebola,wastani
kati ya watu 5 na 9 hufa.Imeonekana kuwa nchi za jirani na Tanzania zimekutwa
na wagonjwa wenye virusi hivyo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni