Tafuta katika Blogu Hii

Jumapili, 7 Oktoba 2018

Tuige mfano wa Chaurembo


Wito huu umetolewa na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM, Wilaya ya Temeke Ndugu: AL Mish Hazal na kutaka Madiwani wote wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Temeke Kuiga mfano wa Mh: Chaurembo, ambaye ni Mstahiki Meya wa Manispaa ya Temeke na Diwani ya kata ya Charambe, kwa kazi nzuri aliyoifanya ya kutoa Semina elekezi kwa mabalozi wa mashina alisema "semina hizi ziende kwenye kata zote za Wilaya ya Temeke".
Akitoa salamu za utangulizi, Ndugu AL Mish, alimpongeza Mh: Chaurembo leo October 07, 2018 katika semina ya mabalozi wa mashina 63 kata ya Charambe katika Ukumbi wa Iramba na kusisitiza kuwa Mstahiki anafaa kuigwa kwa kazi nzuri anazofanya.
"Ninafahamu ya kwamba Charambe ni ngome ya CCM, Mh: Chaurembo ambaye ni Diwani wenu anafanya kazi kubwa sana, Ninafuraha sana kuona na kusikia hali ya siasa katika eneo la Charambe ipo imara...
Kazi kubwa imefanyika kukiimarisha Chama,hongera sana Mh: Chaurembo."
Akigusia mchango na umuhimu wa mabalozi wa mashina katika kukiimarisha Chama cha Mapinduzi CCM, Ndugu AL Mish alisema "Mimi nimekuwa nikiguswa sana na mabalozi wa mashina, mabalozi ni chachu ya ustawi wa chama, nitaendelea kuwaunga mkono na kushirikiana nao katika kukiimarisha chama"alisisitiza.
Ndugu AL Mish aliwasihi mabalozi hao wa mashina wanapofanya vikao vyao vya dharura wampatie mwaliko ili aweze kuona jinsi gani wanavyoendesha vikao.
Vile vile aliwataka waweze kutafakari maelekezo wanayopewa na viongozi wao, Pia wawe na mikakati mizuri ya kuhakikisha Chama cha Mapinduzi CCM kinaibuka na ushindi katika chaguzi za Serikalk za mitaa 2019.
AL Mish aliwataka mabalozi hao wa mashina wawe makini na Wanachama mamluki wanaokuja kujiandikisha na kujifanya ni wana CCM.
Mwisho ndugu AL Mish Hazal aliwataka mabalozi wa mashina wawe na mfuko wa fedha pia wawe na sera ya uwekezaji.
alitoa wito kwa wanachama wa CCM kujichangisha fedha na kuweka kwenye mfuko wa fedha ili chama kiweze kujitegemea katika chaguzi mbalimbali.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

TEMEKE BILA UCHAFU INAWEZEKANA.

MKUU WA WILAYA YA TEMEKE APOKEA MAPIPA ZAIDI YA 241 KWA AJILI YA KAMPENI YA “TEMEKE BILA UCHAFU INAWEZEKANA” Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mh F...