Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke Nassib Mbaga amekifunga kituo cha mabasi yaendayo maeneo ya Jaribu,Ikwilili,Rufiji na maeneo mengine ya mkoa pwani kutokana na mmiliki kutokulipa kodi serikalini kwa miaka tisa.
Mkurugenzi amesema amefunga kituo hicho kutokana na mmiliki wake kwenda kinyume cha taratibu za mmiliki wa biashara pia mmiliki huyo alikuwa akiendesha biashara hiyo bila kuwa na hati halali ya biashara jambo lililosababisha akwepe kulipa kodi ya serikali.Mkurugenzi amesema eneo hilo linatambulika kuwa ni kiwanda namba 19 lakini mmiliki huyo amegeuza kituo cha mabasi ya abiria na eneo la biashara.Mkurugenzi amewaomba Madereva watumie kituo cha Mbagala Rangi Tatu wakati taratibu nyingine za kiofisi zinafanyika kutafuta eneo kubwa kwa ajili ya kituo cha daladala katika wilaya hii.
NASSIB MMBAGA.
MKURUGENZI MANISPAA YA TEMEKE.
Mkurugenzi aliongeza kuwa mmiliki eneo hili amekuwa akiingiza sh.milioni 100 kama kodi,lakini serikali haipati hata shilingi moja kutoka kwa mmiliki huyo.
Mkurugenzi amewaomba radhi wananchi waliokuwa wanatumia kituo hicho kwa usumbufu utakaojitokeza na pia amewaomba wawe wavumilivu wakati huu Manispaa inapolitafutia ufumbuzi kituo hicho.
Tafuta katika Blogu Hii
Jumatano, 2 Novemba 2016
Ijumaa, 28 Oktoba 2016
MKUU WA WILAYA YA TEMEKE AAINISHA MAENEO RASMI YA KUFANYIA BIASHARA.
Mkuu wa wilaya ya Temeke Bw. Felix Jackson Lyaniva ameainisha maeneo rasmi ya kufanyia biashara ndogondogo na kuwataka wafanyabiashara wadogowadogo maarufu kama wamachinga wanaofanya biashara zao nje ya maeneo rasmi kuhamia na kufanyia biashara katika maeneo yafuatayo
Mkuu wa Wilaya ya Temeke Bw.Felix Jackson Lyaniva.
Toangoma kata ya Toangoma, Kilamba kata ya Charambe, Kiponza kata ya Chamazi, Kibondemaji kata ya kibondemaji, Mangaya kata ya Chamazi(Mwembe Pacha), Makangarawe kata ya Makangarawe, Buza kata ya Buza na Sigara lililopo kata ya Yombo Vituka.
Jumamosi, 1 Oktoba 2016
Makamu wa Rais ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan amezindua rasmi Kampeni ya Mti wangu.
Uzinduzi huo umefanyika katika Barabara ya Kilwa wilayani Temeke.
Katika uzinduzi huo Makamu wa Rais amesema kila mmoja wetu ana jukumu la kupanda miti na kuitunza ili kuweza kuhifadhi mazingira pamoja na kukabiliana na mabadilko ya tabia ya nchi pamoja na mabadiliko ya hali ya hewa kwa ujumla.
Ameongeza kwa kusema kuwa Mazingira yetu kwa kiasi kikubwa yanahitaji uthubutu wa kila mmoja wetu kuyahifadhi ili kukabiliana na changamoto za Mbalimali zinazotokana na uharibifu wa Mazingira.akitolea mfano Mvua tukizihitzji haziji kwa wakati,au Kunyesha kupita kiwango jambo ambalo husababisha mafuriko na hivyo kuleta maafa kwa binadam.
Uzinduzi huo umefanyika katika Barabara ya Kilwa wilayani Temeke.
Katika uzinduzi huo Makamu wa Rais amesema kila mmoja wetu ana jukumu la kupanda miti na kuitunza ili kuweza kuhifadhi mazingira pamoja na kukabiliana na mabadilko ya tabia ya nchi pamoja na mabadiliko ya hali ya hewa kwa ujumla.
Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan akizungumza na wananchi kaika Uzinduzi Kampeni ya Mti wangu uliofanyika katika Barabara Kilwa Temeke. |
Jumatano, 21 Septemba 2016
TEMEKE KUPANDA MITI ZAIDI YA 12000 OCTOBA MOSI
Mkuu wa Mkoa wa Dar-es-Salaam Bw.Poul Makonda amefanya ziara ya ukaguzi wa maeneo yaliopo katika Wilaya ya Temeke ambayo yatahusika katika zoezi zima la upandaji wa miti mnamo tarehe 1 ya Mwezi wa 10.
Bwana Makonda amesema zoezi hilo ni la Mkoa mzima wa Dar-es-salaam na anawaomba wananchi wa Mkoa wa Dar-es-salaam kujitokeza kwa wingi ili kushiriki katika zoezi hilo.
Nae Mkuu wa wilaya ya Temeke Bw Felix Jackson Lyaniva amesema Temeke inatarajia kupanda miti zaidi ya elfu kumi na mbili katika siku hiyo.Lyaniva amesema Temeke imejipanga kuhakikisha zoezi hilo linafanikiwa kwa asilimia kubwa pia Mkuu wa wilaya amewaomba wananchi wa Temeke kuhakikisha wanashiriki zoezi hilo kwa walau kila mkazi wa Temeke kuhakikisha anapanda miti walau miwili katika mazingira ya nyumba anayoishi.

Ijumaa, 26 Agosti 2016
Manispaa ya Temeke Kuondoa Kero zilizogundulika Stendi ya Mbagala.
Halmashauri ya Manispaa ya Temeke itafanya operesheni kabambe katika Stendi ya Mbagala lengo likiwa ni kuhakikisha kuwa biashara zote zinafanyika kwenye maeneo yaliyotengwa na salama kwa afya ya jamii. Hayo yalisemwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke Nassib Mbaga na kuagiza wafanyabiashara wanaofanya biashara zao katika eneo hilo kuacha kwani ni kinyume cha taratibu na sheria. ''Tumeandaa operesheni ya kuondoa kero zilizogundulika katika stendi ya Mbagala ili kuhakikisha kuwa biashara zote zinafanyika katika maeneo yaliyopangwa kwa shughuli hizo.
Mbaga alieleza kuwa kuna maeneo matano ambayo yametengwa rasmi kwa ajili ya biashara kama vile Soko la Toangoma, Sigara, Kiponza na Makangarawe, maeneo hayo yakiwa na huduma zote za kijamii ikiwepo vyoo bora.
Aliongeza kuwa Halmashauri imetenga maeneo kwa ajili Masoko ikiwa ni pamoja na Temeke stereo, Vetenari Tazara, Madenge, Tandika kuu, Tandika Kampochea, Keko Magurumbashi, Temeke mwisho, Bulyaga, Kizuani, Zakheem, Mbagala rangi, Mtoni Mtongani, Lumo,Urassa, Feri, Maguruwe,Kabuma na Limboa.
Pia Mkurugenzi aliongeza kuwa Halmashauri imekua ikifanya jitahada za wazi za kuimarisha usafi wa mazingira ya stendi ya Mbagala rangi tatu kwa kufanya ukaguzi wa mara kwa mara ili kuhakikisha eneo hilo pamoja na maeneo yanayozunguka yanakuwa katika hali ya usafi ili kuwa epusha wananchi na magonjwa ya milipuko haswa kipindupindu.

Maafisa Afya wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke wakiwa kwenye ukaguzi wa wafanya bisahara ya vyakula katika kituo cha Mabasi cha Mbagala Rangi Tatu.(picha na Mathew Jonas) |
Aliongeza kuwa Halmashauri imetenga maeneo kwa ajili Masoko ikiwa ni pamoja na Temeke stereo, Vetenari Tazara, Madenge, Tandika kuu, Tandika Kampochea, Keko Magurumbashi, Temeke mwisho, Bulyaga, Kizuani, Zakheem, Mbagala rangi, Mtoni Mtongani, Lumo,Urassa, Feri, Maguruwe,Kabuma na Limboa.
Pia Mkurugenzi aliongeza kuwa Halmashauri imekua ikifanya jitahada za wazi za kuimarisha usafi wa mazingira ya stendi ya Mbagala rangi tatu kwa kufanya ukaguzi wa mara kwa mara ili kuhakikisha eneo hilo pamoja na maeneo yanayozunguka yanakuwa katika hali ya usafi ili kuwa epusha wananchi na magonjwa ya milipuko haswa kipindupindu.
Ijumaa, 19 Agosti 2016
Shule ya Sekondari Kisarawe ii.
Shule ya Sekondari Kisarawe ii ni moja kati ya shule zinazopatikana katika wilaya Mpya ya Kigamboni.
Shule hii ilianzishwa mwaka 2006 ikiwa na vyumba viwili tu vya madarasa,na tangu kuanzishwa kwa shule hii imekuwa mkombozi kwa wanafunzi wengi wanaotoka maeneo ya Mbagala,Kigamboni,Kongowe,na sehemu nyingine tofauti za Manispaa ya Temeke.kitengo cha Habari na Mahusiano cha Manispaa ya Temeke kilifika shuleni hapo ili kuweza kutambua changamoto zinazopatikana shuleni hapo.
Changamoto kubwa ambayo wanafunzi wengi wa shule hiyo waliizungumzia sana ni Usafiri wa kufika shuleni hapo kwa wanafunzi wanakaa maeneo ya Mbagala wanafunzi hao walisema hulazimika kutembea umbali wa kilometa 13 kila siku asubuhi jambo ambalo huwafanya wafike shuleni wakiwa wamechelewa na hivyo kukosa baadhi ya vipindi hasa vipindi vya asubuhi,na wengine hulazimika kupanda malori ya Mchanga ambayo huelekea katika machimbo ya mchanga yaliyopo katika maeeneo ya Kisarewe ii Jambo ambalo huatarisha maisha yao hasa kwa watoto wakike ambao wao wamedai hukutana na changamoto zaidi wanapopanda malori hayo kwani kuna baadhi ya Madereva ama Matingo wa malori hayo ambao si wastaarabu huwaomba namba za simu na wengine hukataa kuwashusha mpaka wawaachie namba za simu.Ili kukabiliana na Changamoto hiyo uongozi wa shule hiyo ukishirikiana na TASAF ulifanikiwa kujenga bweni la Wasichana,lakini bado tatizo hilo limeendelea na hii imetokana na ongezeko la wanafunzi shuleni hapo hivyo shule kushindwa kuwaweka wanafunzi wote katika bweni hilo kutoka na udogo wa bweni hilo.
Mwalimu mkuu wa shule hiyo anasema ilibidi kuanzisha bweni kwa Wasichana japokuwa shule ni ya kutwa ili kujaribu kuwapunguzia wasichana hao changamoto kubwa ya usafiri waliokua wakikutana nayo,na kwa upande wa wavulana Mwalimu Mkuu alisema ilibidi kuiomba baadhi ya madarasa katika shule ya Msingi iliopo jirani na shule hiyo na kuyafanyia ukarabati kupitia Mfuko wa mkuu wa mkoa ili kuwawezesha na wavulana kupata bweni.
Mwalimu mkuu wa shule hiyo anasema anaiomba Halmashauri ya Manispaa ya Temeke pamoja na Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni ambayo ni mpya zimsaidie katika swala zima kuangalia ni jinsi gani wataweza kuongeza Mabweni katika shule hiyo ili kuwawezesha wanafunzi wote wa shule hiyo kukaa bweni.Pia mkuu huyo wa shule aliomba Uongzi wa Manispaa ya Temeke na Kigamboni kwenda kumtatulia tatizo la mipaka kwani kuna ambao wanaanza kuingilia maeneo ya shule hiyo.
Shule hii ilianzishwa mwaka 2006 ikiwa na vyumba viwili tu vya madarasa,na tangu kuanzishwa kwa shule hii imekuwa mkombozi kwa wanafunzi wengi wanaotoka maeneo ya Mbagala,Kigamboni,Kongowe,na sehemu nyingine tofauti za Manispaa ya Temeke.kitengo cha Habari na Mahusiano cha Manispaa ya Temeke kilifika shuleni hapo ili kuweza kutambua changamoto zinazopatikana shuleni hapo.
Changamoto kubwa ambayo wanafunzi wengi wa shule hiyo waliizungumzia sana ni Usafiri wa kufika shuleni hapo kwa wanafunzi wanakaa maeneo ya Mbagala wanafunzi hao walisema hulazimika kutembea umbali wa kilometa 13 kila siku asubuhi jambo ambalo huwafanya wafike shuleni wakiwa wamechelewa na hivyo kukosa baadhi ya vipindi hasa vipindi vya asubuhi,na wengine hulazimika kupanda malori ya Mchanga ambayo huelekea katika machimbo ya mchanga yaliyopo katika maeeneo ya Kisarewe ii Jambo ambalo huatarisha maisha yao hasa kwa watoto wakike ambao wao wamedai hukutana na changamoto zaidi wanapopanda malori hayo kwani kuna baadhi ya Madereva ama Matingo wa malori hayo ambao si wastaarabu huwaomba namba za simu na wengine hukataa kuwashusha mpaka wawaachie namba za simu.Ili kukabiliana na Changamoto hiyo uongozi wa shule hiyo ukishirikiana na TASAF ulifanikiwa kujenga bweni la Wasichana,lakini bado tatizo hilo limeendelea na hii imetokana na ongezeko la wanafunzi shuleni hapo hivyo shule kushindwa kuwaweka wanafunzi wote katika bweni hilo kutoka na udogo wa bweni hilo.
Majengo ya Madrasa Shule ya Sekondari Kisarawe ii |
Jengo la bweni la Wasichana la Shule ya Sekondari Kisarawe ii. |
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)
TEMEKE BILA UCHAFU INAWEZEKANA.
MKUU WA WILAYA YA TEMEKE APOKEA MAPIPA ZAIDI YA 241 KWA AJILI YA KAMPENI YA “TEMEKE BILA UCHAFU INAWEZEKANA” Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mh F...
-
Shule ya Sekondari Kisarawe ii ni moja kati ya shule zinazopatikana katika wilaya Mpya ya Kigamboni. Shule hii ilianzishwa mwaka 2006 ikiwa...
-
TEMEKE YAKABIDHIWA MABENCHI KUTOKA GOODONE Halmashauri ya Manispaa ya Temeke yakabidhiwa mabenchi kutoka kampuni ya ...