Tafuta katika Blogu Hii

Jumatatu, 31 Julai 2017


KATIBU TAWALA TEMEKE AHAMASISHA MICHEZO TEMEKE.
Katika kuhamisha michezo Temeke, Katibu Tawala Wilaya ya Temeke Mh. Hashimu Komba awapongeza Team ya Keko Furniture ambayo imefanikiwa kuingia nusu fainali ya Ndondo Cup katika mechi iliyochezwa dhidi ya Timu ya Stimutosha fc na kujipatia ushindi wa penalti(matuta). Aidha Mh; Komba amewapongeza sana timu ya Keko Furniture kwa kufanikiwa kuingia hatua ya nusu fainali


 Katibu tawala wa wilaya ya Temeke Bw.Hashimu Komba akizungunmza na wachezeji wan timu ya Keko furniture.

wachezaji na viongozi wa timu ya Keko Furniture wakimsikiliza katibu tawala wa wilaya Temeke Bw Hashimu Komba hayupo pichani.

Mashindano hayo yaliyobeba kauli mbiu ya "kamatia kombe Temeke" yanalenga kulitetea kombe hilo ambalo limekua wilayani humo kwa muda mrefu. Mh; DAS ameahidi kutoa kiasi cha fedha TSH; 50000/= kwa kila goli watakalo pata. Pia ametoa hamasa kwa wadau wote wa Temeke kudhamini team hiyo ili kujiletea ushindi nyumbani na kuondoa baadhi ya changamoto wanazokutana nazo.
katika hatua hiyo diwani wa kata ya keko Mh; Fundi Shabani kwaniaba ya madiwani wote wa wilaya ya Temeke amehaidi kuwaweka kambini team hiyo kwa muda wa siku mbili  na kuwapatia chakula na usafiri endapo watavuka nusu fainali. Pia Masai Recording Picture nao wameahidi kutoa usafiri na chakula kwa mechi zote zilizobaki ,na kiasi cha fedha elfu hamsini, 50000/= kwa kila goli watakalo funga.

Timu ya keko funiture ni miongoni mwa timu iliyofanikiwa kufanya vizuri katika mashindano ya NdoNdo Cup mwaka huu katika wilaya ya Temeke, kila la kheri katika kunyakua ubingwa Keko Furniture Team

Ijumaa, 28 Julai 2017

MANISPAA YA TEMEKE NANENANE MAMBO NI MOTO.
Manispaa ya Temeke inakukaribisha wewe mwananchi kujifunza na kupata maelezo mbalimbali ya kitaalam yanayohusu kilimo na ufugaji katika banda letu lililopo viwanja vya nanenane mjini Morogoro, karibuni nyote.





Alhamisi, 27 Julai 2017

                     TEMEKE YAKABIDHIWA MABENCHI KUTOKA GOODONE

Halmashauri ya Manispaa ya Temeke yakabidhiwa mabenchi kutoka kampuni ya Goodone,mabenchi hayo yalipokelewa na katibu tawala wilaya Mh Hashim Komba ambapo amepokea mabenchi 30 kwa ajili ya matumizi ya wagonjwa hususani wajawazito katika kitengo cha huduma ya uzazi, mama na mtoto katika hospitali ya Mbagala Rangi tatu na Kampuni ya Goodone. Aidha misaada hiyo imelenga pia kusaidia kituo cha afya kata ya Yombo, hospitali ya Yombo vituka.
Sambamba na hilo, kampuni ya Goodone imetoa sabuni za kufulia mashuka ya hospitali hizo. Misaada hiyo imegharimu jumla ya Tsh Milioni 12.
Mganga Mfawidhi wa hospitali ya Mbagala Rangi Tatu DK. Joseph Kaini amewashukuru wadau wote na mkurugenzi Mkuu wa Goodone ambaye ameonyesha nia ya kusaidia zaidi hospitali..


Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya GOODONE

Mabenchi yaliyotolewa na kampuni ya GOODONE

Mganga mfawidhi Dk.Joseph Kaini akizungumza  na uongozi wa GOODONE 

Mh DAS akipokea moja kati ya mabenchi yaliyotolewa na kampuni GOODONE (katikati),Mr.WU mkurugenzi mkuu GOODONE(kushoto) Dr.Joseph kain(kulia)

Mh DAS akitoa shukrani kwa uongozi  wa kampuni ya GOODONE kwa niaba ya wananchi

Miongoni mwa msaada wa sabuni zilizotolewa na GOODONE

Wananchi wa Mbagala wakijitokeza kupokea misaada hiyo

Jumatatu, 10 Julai 2017

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angella Kairuki, ameanza ziara yake Mkoa wa Dar es Salaam kwa lengo kuzifahamu changamoto mbalimbali za watumishi na kutoa maelekezo ya kutatua kero hizo.
Katika ziara yake ambayo ameanza na Wilaya ya Temeke Waziri Kairuki ameagiza uanzishwaji wa vituo vya kusaidia upatikanaji wa huduma kwa wakati maarufu kama 'One Stop Center' katika idara ya Mamlaka ya Mapato (TRA) na idara ya Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), ili kuongeza ufanisi wa kazi na ukusanyaji wa kodi kwa wakati, halkadhalika uwepo usajili wa biashara kwa haraka ambapo itasaidia katika Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania maarufu kama “MKURABITA”

Katika hatua nyingine Waziri Kairuki ametoa msisitizo kwa Maafisa Utumishi kuhakikisha serikali inapotoa vibali vya kazi, hawaajiri watu bila kujiridhisha na taarifa zao za kielimu ili kuepuka suala la watumishi wenye vyeti feki, ambapo ameeleza kuwa kwa mujibu wa taarifa iliyowakilishwa na Katibu Tawala Msaidizi Michael Mungaya wa Mkoa wa Dar es Salaam imeeleza kuwa watumishi 937 wanavyeti feki na katika hao 421 wameleta vyeti pungufu, ni vyema umakini ukafanyika ili kuondoa hasara kwa taifa.

Jumatatu, 3 Julai 2017

Waziri Mkuu Majaliwa K. Majaliwa azindua Uzinduzi wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini uliofanyika Kwenye Ukumbi wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere uliopo katika Chuo Cha Mipango Mjini Dodoma

Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke Jijini Dar es salaam Ndg Nassib Mbaga ameungana na wakurugenzi wengine nchini kuhudhuria Mkutano wa Uzinduzi wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini uliofanyika Kwenye Ukumbi wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere uliopo katika Chuo Cha Mipango Mjini Dodoma.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke Nassib Mbaga  ameshiriki Mkutano huo uliofunguliwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Kassim  Majaliwa,wenye dhamira ya kuleta mageuzi makubwa katika sekta ya Barabara nchini kutokana na kuanzishwa kwa wakala wa barabara Mijini na Vijijini.

Uanzishwaji wa Wakala wa Barabara nchini ni utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya Mwaka 2015 iliyopo katika ukurasa wa 54 inayoielekeza serikali kuanzisha Wakala/Taasisi itakayosimamia kazi za ujenzi na matengenezo ya barabara za Halmashauri, Miji, na Majiji ambazo zipo chini ya TAMISEMI ifikapo mwaka 2020.

                 Majliwa Kassim Majaliwa .Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania

Katika Mkutano huo zimeelezwa changamoto mbalimbali zinazozikabili mamlaka za serikali za Mitaa katika ujenzi, ukarabati na matengenezo ya miundombinu ya Barabara ambazo ni pamoja na Miradi kutekelezwa kwa viwango duni, Ucheleweshaji wa utekelezaji wa miradi kutokana na mipango isiyoridhisha, Kandarasi kutolewa bila kuzingatia vigezo, uwezo na sifa.
Changamoto zingine ni pamoja na kutokuwepo kwa viwango vinavyoshabihiana vya ubora wa barabara Kati ya Halmashauri Moja na nyingine, Fedha zilizopangwa kutekeleza miradi ya barabara kutotumika kutokana na urasimu wa viongozi wa Halmashauri,Rushwa iliyokithiri katika utoaji wa zabuni, Mgongano wa maslahi na usimamizi hafifu wa mikataba ya ujenzi.
Wakala huu utasaidia kuimarisha mtandao wa barabara za vijijini na hivyo kuwawesesha wananchi wengi zaidi kusafiri na kusafirisha bidhaa za mashambani kwa urahisi.
Katika Mkutano huo Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Majaliwa K. Majaliwa akizungumza kabla ya kuzindua Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini alieleza manufaa yatakayopatikana kutokana na kuwa na Barabara za Vijijini na Mijini kuwa ni pamoja na kuongeza chachu ya uzalishaji Mali mashambani kutokana na urahisi wa kufikisha mazao sokoni, Kushusha bei ya vyakula mijini kutokana na gharama za kusafirisha mazao kutoka mashambani kupungua.
Mengine ni kuboresha na kubadili hali za kimaisha na kiuchumi kwa wananchi, kufanya maeneo mengi zaidi ya nchi kufikika kwa urahisi na hivyo kuboresha utoaji wa huduma za kijamii na Kutoa ajira kwa vijana katika maeneo ambayo ujenzi au ukarabati wa miundombinu utakapokuwa unafanyika.
Katika Mkutano huo Halmashauri ya Manispaa ya Temeke,imewakilishwa na Mkurugenzi Nassib Mbaga ambaye ameambatana na Mkuu wa Idara ya Ujenzi na Zimamoto Manispaa ya Temeke Ndg Nicolas Francis.

TEMEKE BILA UCHAFU INAWEZEKANA.

MKUU WA WILAYA YA TEMEKE APOKEA MAPIPA ZAIDI YA 241 KWA AJILI YA KAMPENI YA “TEMEKE BILA UCHAFU INAWEZEKANA” Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mh F...