Waziri
Mkuu Majaliwa K. Majaliwa azindua Uzinduzi wa Wakala wa Barabara za Vijijini na
Mijini uliofanyika Kwenye Ukumbi wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere uliopo
katika Chuo Cha Mipango Mjini Dodoma
Mkurugenzi
wa Manispaa ya Temeke Jijini Dar es salaam Ndg Nassib Mbaga ameungana na
wakurugenzi wengine nchini kuhudhuria Mkutano wa Uzinduzi wa Wakala wa Barabara
za Vijijini na Mijini uliofanyika Kwenye Ukumbi wa Mwalimu Julius Kambarage
Nyerere uliopo katika Chuo Cha Mipango Mjini Dodoma.
Mkurugenzi
wa Manispaa ya Temeke Nassib Mbaga ameshiriki Mkutano huo uliofunguliwa na Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Kassim Majaliwa,wenye dhamira ya kuleta mageuzi
makubwa katika sekta ya Barabara nchini kutokana na kuanzishwa kwa wakala wa
barabara Mijini na Vijijini.
Uanzishwaji
wa Wakala wa Barabara nchini ni utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya Chama Cha
Mapinduzi (CCM) ya Mwaka 2015 iliyopo katika ukurasa wa 54 inayoielekeza
serikali kuanzisha Wakala/Taasisi itakayosimamia kazi za ujenzi na matengenezo
ya barabara za Halmashauri, Miji, na Majiji ambazo zipo chini ya TAMISEMI
ifikapo mwaka 2020.
Majliwa Kassim Majaliwa .Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania
Katika
Mkutano huo zimeelezwa changamoto mbalimbali zinazozikabili mamlaka za serikali
za Mitaa katika ujenzi, ukarabati na matengenezo ya miundombinu ya Barabara
ambazo ni pamoja na Miradi kutekelezwa kwa viwango duni, Ucheleweshaji wa
utekelezaji wa miradi kutokana na mipango isiyoridhisha, Kandarasi kutolewa
bila kuzingatia vigezo, uwezo na sifa.
Changamoto
zingine ni pamoja na kutokuwepo kwa viwango vinavyoshabihiana vya ubora wa
barabara Kati ya Halmashauri Moja na nyingine, Fedha zilizopangwa kutekeleza
miradi ya barabara kutotumika kutokana na urasimu wa viongozi wa Halmashauri,Rushwa
iliyokithiri katika utoaji wa zabuni, Mgongano wa maslahi na usimamizi hafifu
wa mikataba ya ujenzi.
Wakala
huu utasaidia kuimarisha mtandao wa barabara za vijijini na hivyo kuwawesesha
wananchi wengi zaidi kusafiri na kusafirisha bidhaa za mashambani kwa urahisi.
Katika
Mkutano huo Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Majaliwa K.
Majaliwa akizungumza kabla ya kuzindua Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini
alieleza manufaa yatakayopatikana kutokana na kuwa na Barabara za Vijijini na
Mijini kuwa ni pamoja na kuongeza chachu ya uzalishaji Mali mashambani kutokana
na urahisi wa kufikisha mazao sokoni, Kushusha bei ya vyakula mijini kutokana
na gharama za kusafirisha mazao kutoka mashambani kupungua.
Mengine
ni kuboresha na kubadili hali za kimaisha na kiuchumi kwa wananchi, kufanya
maeneo mengi zaidi ya nchi kufikika kwa urahisi na hivyo kuboresha utoaji wa
huduma za kijamii na Kutoa ajira kwa vijana katika maeneo ambayo ujenzi au
ukarabati wa miundombinu utakapokuwa unafanyika.
Katika
Mkutano huo Halmashauri ya Manispaa ya Temeke,imewakilishwa na Mkurugenzi
Nassib Mbaga ambaye ameambatana na Mkuu wa Idara ya Ujenzi na Zimamoto Manispaa
ya Temeke Ndg Nicolas Francis.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni