Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angella Kairuki, ameanza ziara yake Mkoa wa Dar es Salaam kwa lengo kuzifahamu changamoto mbalimbali za watumishi na kutoa maelekezo ya kutatua kero hizo.
Katika ziara yake ambayo ameanza na Wilaya ya Temeke Waziri Kairuki ameagiza uanzishwaji wa vituo vya kusaidia upatikanaji wa huduma kwa wakati maarufu kama 'One Stop Center' katika idara ya Mamlaka ya Mapato (TRA) na idara ya Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), ili kuongeza ufanisi wa kazi na ukusanyaji wa kodi kwa wakati, halkadhalika uwepo usajili wa biashara kwa haraka ambapo itasaidia katika Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania maarufu kama “MKURABITA”
Katika hatua nyingine Waziri Kairuki ametoa msisitizo kwa Maafisa Utumishi kuhakikisha serikali inapotoa vibali vya kazi, hawaajiri watu bila kujiridhisha na taarifa zao za kielimu ili kuepuka suala la watumishi wenye vyeti feki, ambapo ameeleza kuwa kwa mujibu wa taarifa iliyowakilishwa na Katibu Tawala Msaidizi Michael Mungaya wa Mkoa wa Dar es Salaam imeeleza kuwa watumishi 937 wanavyeti feki na katika hao 421 wameleta vyeti pungufu, ni vyema umakini ukafanyika ili kuondoa hasara kwa taifa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni