Tafuta katika Blogu Hii

Jumatatu, 31 Julai 2017


KATIBU TAWALA TEMEKE AHAMASISHA MICHEZO TEMEKE.
Katika kuhamisha michezo Temeke, Katibu Tawala Wilaya ya Temeke Mh. Hashimu Komba awapongeza Team ya Keko Furniture ambayo imefanikiwa kuingia nusu fainali ya Ndondo Cup katika mechi iliyochezwa dhidi ya Timu ya Stimutosha fc na kujipatia ushindi wa penalti(matuta). Aidha Mh; Komba amewapongeza sana timu ya Keko Furniture kwa kufanikiwa kuingia hatua ya nusu fainali


 Katibu tawala wa wilaya ya Temeke Bw.Hashimu Komba akizungunmza na wachezeji wan timu ya Keko furniture.

wachezaji na viongozi wa timu ya Keko Furniture wakimsikiliza katibu tawala wa wilaya Temeke Bw Hashimu Komba hayupo pichani.

Mashindano hayo yaliyobeba kauli mbiu ya "kamatia kombe Temeke" yanalenga kulitetea kombe hilo ambalo limekua wilayani humo kwa muda mrefu. Mh; DAS ameahidi kutoa kiasi cha fedha TSH; 50000/= kwa kila goli watakalo pata. Pia ametoa hamasa kwa wadau wote wa Temeke kudhamini team hiyo ili kujiletea ushindi nyumbani na kuondoa baadhi ya changamoto wanazokutana nazo.
katika hatua hiyo diwani wa kata ya keko Mh; Fundi Shabani kwaniaba ya madiwani wote wa wilaya ya Temeke amehaidi kuwaweka kambini team hiyo kwa muda wa siku mbili  na kuwapatia chakula na usafiri endapo watavuka nusu fainali. Pia Masai Recording Picture nao wameahidi kutoa usafiri na chakula kwa mechi zote zilizobaki ,na kiasi cha fedha elfu hamsini, 50000/= kwa kila goli watakalo funga.

Timu ya keko funiture ni miongoni mwa timu iliyofanikiwa kufanya vizuri katika mashindano ya NdoNdo Cup mwaka huu katika wilaya ya Temeke, kila la kheri katika kunyakua ubingwa Keko Furniture Team

Maoni 2 :

  1. Hongereni Keko Furniture team kila la heri mkanyakue ushindi. Mheshimiwa DAS na mheshimiwa diwani hongereni kwa kuwatia moyo vijana.

    JibuFuta
  2. Hongereni Keko Furniture team kila la heri mkanyakue ushindi. Mheshimiwa DAS na mheshimiwa diwani hongereni kwa kuwatia moyo vijana.

    JibuFuta

TEMEKE BILA UCHAFU INAWEZEKANA.

MKUU WA WILAYA YA TEMEKE APOKEA MAPIPA ZAIDI YA 241 KWA AJILI YA KAMPENI YA “TEMEKE BILA UCHAFU INAWEZEKANA” Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mh F...