Tafuta katika Blogu Hii

Ijumaa, 6 Oktoba 2017

JUKWAA LA WANAWAKE WAJASILIAMALI TEMEKE LAUNDWA

JUKWAA LA WANAWAKE WAJASILIAMALI TEMEKE LAUNDWA

Katibu Tawala Wilaya ya Temeke Bw:Hashimu Komba aunda jukwaa la wanawake wajasiliamali wa wilaya ya Temeke ambao walijitokeza kwa wingi kutoka kata zote za wilaya hiyo. Akiongea na wanawake hao wajasiliamali leo katika ukumbi wa Iddi Nyundo Manispaa ya Temeke.



               Pichani Bw:Hashimu Komba, Katibu Tawala Wilaya ya Temeke.


kauli mbiu ya kikao hicho ni “Mwanamke tumia fursa kuimalisha uchumi wa viwanda” ambapo Katibu tawala huyo ameungana na juhudi za Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu ikiwa ni mwendelezo wa uzinduzi wa jukwaa la wanawake katika kuinua uchumi wa mwanamke ili kuleta Maendeleo ya taifa kiwilaya.
Kauli mbiu hiyo ilisemwa na Makamu wa Rais katika siku ya uzinduzi wa Jukwaa la uwezeshaji wa wanawake kiuchumi kimkoa lililofanyika katika viwanja vya Posta,kijtonyama. Ambapo uzinduzi huo ni wa 23,lililoandaliwa na Baraza la uwezeshaji kwa ufadhili wa benki ya CRDB.
Komba aliwamwagia sifa wanawake kwa juhudi zao za kujikwamua kiuchumi katika jamii,aliwapongeza akina mama kwanamna wanavyojituma na kuwa waaminifu na kuwa na uwezo wa kusimamia vipato vyao vidogo wanavyopata kwa kujileta maendeleo makubwa.



  
 Pichani watumishi wa Manispaa na wanawake wajasiliamali wakimsikiliza        Bw:DAS kwa makini.


Ahadi kuwa jukwaa hilo punde litakopo undwa litakuwa na tija kubwa katika kujitangazia biashara na ubunifu wa kazi zao wanazofanya katika ngazi za kimataifa,kitaifa,kimkoa,kiwilaya mpaka kata. Pia watapata fursa mbalimbali za kupiga hatua kama kushiriki maonesho ya kibiashara ya sabasaba na nanenane. Hivyo asisitiza kuchaguliwa kwa viongozi walio na uwezo wakusimamia mawazo,ubunifu na ujuzi wa kazi zao ili kusimamia jukwaa hilo katika kujiletea maendeleo.

Hata hivyo amewapa moyo kuwa kuelekea katika sera ya uchumi wa viwanda kwa kuanzia waendelea kutumia technolojia hizo hizo ndogondogo wanazotumia nyumbani kuzalisha bidhaa mbalimbali ikiwa ni mfano wa viwanda vidogovidogo,wakati wanajiandaa kupata viwanda vikubwa. Kwakufanya hivyo watakuwa wanajiingizia kipato,pia kuinua uchumi wa viwanda katika nchi yetu.



Wanawake wajasiliamali wakiwa katika kikao cha uundaji wa jukwaa la wanawake wajasiliamali kiwilaya.


Katika kikao hicho katibu Tawala huyo alipongeza Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii inayoongozwa na John Bwana kwa kazi nzuri wanayoifanya kwa kuwatambua wajasiliamali hao ambao wamejitokeza kwa wingi na shauku kubwa kuunda jukwaa hilo.

Jukwaa hilo linatazamiwa kuzinduliwa hivi karibuni lengo kuu ikiwa ni kumwinua mwanamke kufikia katika uchumi wa kati, ambapo inasemekana mwanamke ni mlezi wa familia na jamii, ukimwezesha mwanamke imeliwezesha taifa.
Top of Form


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

TEMEKE BILA UCHAFU INAWEZEKANA.

MKUU WA WILAYA YA TEMEKE APOKEA MAPIPA ZAIDI YA 241 KWA AJILI YA KAMPENI YA “TEMEKE BILA UCHAFU INAWEZEKANA” Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mh F...