Tafuta katika Blogu Hii

Alhamisi, 30 Novemba 2017

DC TEMEKE ATEMBELEA KITENGO CHA HABARI TEMEKE


Mapema leo mkuu wa wilaya ya Temeke Mh:Felix Lyaniva afanya ziara katika kitengo cha habari Manispaa ya Temeke.

Akiwa katika ziara hiyo aliwapongeza wana kitengo kwa juhudi na ubunifuwao wa kuhabarisha umma kwa wakati na kwa kutumia njia mbalimbali za mitandao ya kijamii vizuri.




Aidha M:Lyaniva alishauri  kudumisha uhusiano mzuri na vyombo vingine vya habari pamoja na taasisi za serikali ili kuongeza wigo mpana wa kufikia wananchi kwa wingi na wakati sahihi.

Hata   hivyo mkuu wa wilaya aliwasihi waendelee kufanya kazi kwa umoja ,weledi na ufanisi mzuri ili jamii iweze kupata habari za uhakika na kwa wakati sahihi.




Kwa habari za uhakika tufatilie kupitia:

Website:  www.temekemc.go.tz
Facebook:  TemekeManispaa
Twitter:  temekeManispaa1
Blog:  manispaatemeke.blogspot.com
Onlinetv: youtube TMCTV

Kwa maoni na ushauri tuandikie kupitia:

Baruapepe:  temeke@temekemc.go.tz

S.L.P 46343 DSM

Jumatano, 29 Novemba 2017

DC TEMEKE AZINDUA KAMATI YA UJENZI


Mh: Felix Lyaniva azindua kamati ya ujenzi wa kituo kisasa cha polisi katika kata ya Chamazi. Katika uzinduzi huo Mh: DC alisema kuimalika kwa ujenzi wa Kituo hicho kutaimarisha ulinzi na kutokomeza vitendo vya uhalifu mbalimbali.

Hata hivyo Mh:DC amewaasa na kuwatia moyo watendaji wa kamati hiyo kufanya kazi kwa weledi,uaminifu na uwazi ili kufikia malengo waliyojiwekea.


Ujenzi wa kituo cha polisi kata ya Chamazi  unajengwa na wadau mbalimbali wa Temeke ili kutokomeza vitendo vya uhalifu na kuweka ulinzi madhubuti  katika kata hiyo.


Jumanne, 28 Novemba 2017




                                 MATOKEO YA UCHAGUZI WA UDIWANI.
Halmashauri ya Manispaa ya Temeke yatangaza Matokeo ya Uchaguzi wa Diwani Kata Ya Kijichi.
Matokeo ya udiwani yametangazwa usiku wa kuamkia leo na msimamizi mkuu Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke Ndugu;Nassib Mbaga, na matokeo yalikua kama ifuatavyo:
ACT WAZALENDO 416
ADC 21
CCM 2658
CUF 916
NCCR MAGEUZI 13
MH.ELISA KASSIM MTALAWANJE AMEIBUKA MSHINDI NA NDIE DIWANI WA KATA YA KIJICHI KUPITIA CCM.


     HOMA YA MATENDE NA MABUSHA  YAFIKIA  MWISHO TEMEKE.

Halmashauri ya Manispaa ya Temeke yazindua rasmi kampeni ya utoaji tiba kinga za matende,busha na minyoo ya tumbo leo. Zoezi hilo linaloendeshwa kitaifa katika ngazi ya Mkoa kila mwaka  kwaajili ya kutoa tiba kinga ya magonjwa yasiyopewa kipaumbele.
Akizungumza mapema leo ofisni kwake mratibu wa magonjwa yasiyopewa kipaumbele ndg; Jumanne Kagoda  amesema ''wananchi wajitokeze kwa wingi  ili waweze kupata tiba kinga ya magonjwa ya matende na mabusha , pia amesisitiza wananchi kuhamasishana ili kujitokeza kwa wingi''.  Amewaasa wananchi  kutokusikiliza maneno ya upotoshwaji mbaya  kuhusu dawa zinazotolewa,kwani  dawa  hizo hazina madhara yoyote kiafya.
Zoezi hili la utoaji dawa kama tiba kinga litahusisha watu wote, wanawake kwa wanaume kuanzia umri wa miaka 5 na kuendelea. Na halitahusisha Wagonjwa mahututi,wajawazito na watoto chini ya miaka 5.
Aidha Halmashauri ya Manispaa ya Temeke imetenga zaidi ya vituo 179 vya kutolea dawa, hivyo wananchi mnaombwa kujitokeza kwa wingi kwani zoezi hilo ni bure kabisa.
''Kinga ni bora kuliko tiba''


TEMEKE BILA UCHAFU INAWEZEKANA.

MKUU WA WILAYA YA TEMEKE APOKEA MAPIPA ZAIDI YA 241 KWA AJILI YA KAMPENI YA “TEMEKE BILA UCHAFU INAWEZEKANA” Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mh F...