HOMA YA MATENDE
NA MABUSHA YAFIKIA MWISHO TEMEKE.
Halmashauri
ya Manispaa ya Temeke yazindua rasmi kampeni ya utoaji tiba kinga za
matende,busha na minyoo ya tumbo leo. Zoezi hilo linaloendeshwa kitaifa katika
ngazi ya Mkoa kila mwaka kwaajili ya
kutoa tiba kinga ya magonjwa yasiyopewa kipaumbele.
Akizungumza
mapema leo ofisni kwake mratibu wa magonjwa yasiyopewa kipaumbele ndg; Jumanne
Kagoda amesema ''wananchi wajitokeze kwa
wingi ili waweze kupata tiba kinga ya
magonjwa ya matende na mabusha , pia amesisitiza wananchi kuhamasishana ili
kujitokeza kwa wingi''. Amewaasa
wananchi kutokusikiliza maneno ya upotoshwaji
mbaya kuhusu dawa zinazotolewa,kwani dawa hizo hazina madhara yoyote kiafya.
Zoezi
hili la utoaji dawa kama tiba kinga litahusisha watu wote, wanawake kwa wanaume
kuanzia umri wa miaka 5 na kuendelea. Na halitahusisha Wagonjwa
mahututi,wajawazito na watoto chini ya miaka 5.
Aidha
Halmashauri ya Manispaa ya Temeke imetenga zaidi ya vituo 179 vya kutolea dawa,
hivyo wananchi mnaombwa kujitokeza kwa wingi kwani zoezi hilo ni bure kabisa.
''Kinga ni bora
kuliko tiba''
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni