MH.LYANIVA AWATAKA WAKAZI WA TEMEKE KATIKA KUELEKEA MSIMU
WA KUFUNGA MWAKA, WASHEREHEKEA KWA UTULIVU NA AMANI.ALIYASEMA HAYO ALIPOKUA AKIFANYA MKUTANO NA WAANDISHI WA HABARI OFISINI KWAKE.
PIA APIGA MARUFUKU UCHOMAJI WA MATAIRI , UPIGAJI BARUTI NA KUFUNGA BARABARA PASIPO KUWA NA SABABU MAALUMU.
HALI KADHALIKA ATOA ONYO KALI KWA WAKWEPA KODI MBALIMBALI,WAHAKIKISHE WANALIPA KODI KWA WAKATI,ALISISITIZA IFIKAPO MWAKANI OPARESHENI MAALUMU ITAENDESHWA MTAA KWA MTAA ILI KUFICHUA WAKWEPA KODI HAO.
SAMBAMBA NA HAYO AMEWASISITIZA WAZAZI KUWAANDIKISHA WATOTO WAO SHULE PINDI IFIKAPO MWAKANI.
MWISHO AMEWATAKIA WATU WOTE KHERI YA MWAKA MPYA.