Mkuu wa Wilaya ya
Temeke Mh:Felix Lyaniva azindua jukwaa la wanawake Kiwilaya katika viwanja vya
Mwembe Yanga. Katika uzinduzi huo DC Lyaniva asisitiza wanawake kupendana,kuwa
na umoja ili kujiletea maendeleo ya kweli,hata kufikia uchumi wa kati.
Wanawake hao ambao
wamejitokeza kwa wingi katika uzinduzi huo, huku sherehe hizo zikipambwa na
shamrashamra za maandamano ya vikundi mbalimbali vya wanawake wajasiriamali.
Pia wanawake
wajasiriamali walionesha kazi za mikono na ubunifu ufanywao na vikundi vyao.
Katika uzinduzi huo
ulifanyika uchaguzi wa mwenyekiti wa jukwaa la wanawake Kiwilaya ambapo Johari
Maulid Mkonde alichaguliwa rasmi kuwa mwenyekiti wa jukwaa la wanawake wilayani
Temeke.
Hata hivyo wanawake
wa Temeke wamepewa fursa kushiriki uchumi wa viwanda ili waweze kufika malengo
ya maendeleo endelevu ya 50/50 ya dunia kufikia mwaka 2030.
Jukwa la wanawake
liliundwa ili kuwawezesha wanawake kiuchumi na kuondoa pengo kubwa ambalo limejengeka
duniani na kuongeza ushiriki wa wanawake katika uchumi duniani kote. Majukwaa
haya yatazinduliwa katika Mikoa yote nchini na Halmashauri zote. Katika Mkoa wa
Dare Es Salaam Wilaya ya Temeke ni Wilaya ya kwanza kuzindua jukwaa la
wanawake.
Kauli mbiu katika
uzinduzi huu ni ''Mwanamke Tumia Fursa
Kushiriki Uchumi wa Viwanda''
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni