Naibu wa Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na
serikali za Mitaa(TAMISEMI) Josephat Kandege afurahishwa na uwazi wa miradi
inayoendelea katika wilaya ya Temeke.
Mh: Kandege amefanya ziara katika Wilaya ya
Temeke ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya miradi ya maendeleo katika Mkoani Dar
Es Salaam. Miradi hiyo ambayo imefadhiliwa na Banki kuu ya Dunia.
Lengo kuu ya ziara yake ni kujiridhisha na utekelezwaji
wa miradi hiyo na kuhakikisha miradi hiyo inakamilika kwa wakati. Pia kukagua
usalama wa wananchi wanaoishi karibu na ujenzi wa miradi hiyo.
Hata hivyo amerizishwa na utendekaji kazi na
kasi ya miradi hiyo inavyoendelea. Ameipongeza ofisi ya Mkurugenzi kwa jinsi
inavyosimamia vizuri mapato na matumizi ya fedha za miradi.
Miradi ambayo imetembelewa ni pamoja na ujenzi
wa jengo la ofisi ya DMDP lilipo katika eneo la Halmashauri ya Manispaa ya
Temeke,ambalo lilmekamilika na kutumika.
Barabara ya Mwanamtoti, Daraja la kijichi Toangoma,Soko
na Stand ya kijichi ambayo yote imefikia katika hatua nzuri. Miradi yote hii
inatarajiwa kukamilika kufikia mwezi wa pili mwakani.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni