Wakuu wa idara na vitengo wa Halmashauri ya
Manispaa ya Temeke wafanya ukaguzi wa
miradi ya maendeleo yenye thamani ya zaidi ya bilioni 3.
Miradi ambayo
inajengwa na vyanzo vya mapatao vya halmashauri ya manispaa yaTemeke. Ambapo
mradi wa kisima cha maji kata ya Azimio mtaa wa Mbuyuni wenye thamani ya zaidi
ya milioni 400 umefadhiliwa na Benki ya Dunia umefikia hatua za mwisho ili wananchi
waanze kupata huduma ya maji.
Miradi hiyo ambayo imetembelewa ni ujenzi wa vyumba
6 vya madarasa Chamazi sekondari, ujenzi wa vyumba 2 vya madarasa shule ya
Msingi Mgeninani, Ukaguzi wa Zahati ya Kijichi, ujenzi wa vyumba 4 vya madarasa
shule ya sekondari Mbagala, ukaguzi wa zahanati Yombo vituka, ujenzi wa vyumba
2 vya madarasa s/Msingi Karume, kukagua mradi wa maji Mabatini, ujenzi wa
vyumba 4 vya madarasa Miburani sekondari.
Mradi wa vyumba vya madarasa katika shule ya
karume na shule ya Msingi Mgeninani imekamilika.
Miradi yote ipo katika hatua nzuri ili kukamilika.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni