Halmashauri inatarajia kujenga jengo
la upasuaji,wodi ya wazazi na mtoto, ukarabati na ujenzi wa Maabara pamoja na
vyumba vya watumishi katika kituo cha afya Yombo Vituka na Zahanati ya
Majimatitu ikiwa na lengo la kuimarisha afya ya mama na mtoto pia kupunguza
vifo vitokanayo na uzazi.
Ujenzi huu unatarajia kukamilika
ifikapo mwezi April na utagharimu jumla ya Shilingi Milioni mia nane(800)
ambapo kituo cha afya Yombo Vituka kitagawiwa kiasi cha Shilingi Millioni Mia
nne (400) na Zahanati ya Majimatitu Shilingi Millioni mia nne(400).
Akizungumza na wafanyakazi wa kituo
cha afya Yombo Vituka wakati wa ziara ya kuangalia matumizi ya fedha
zilizotolewa na Benki ya Dunia, Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bibi Dorothy Mwaluko aliwapongeza sana
watumishi wa Zahanati hiyo pamoja na Kamati mbalimbali, kwa kujitoa kwao na
kuhakikisha ujenzi unatekelezeka bila kuwa na malalamiko wala migongano. Pia
uwazi umeonekana wa hali ya juu na kuwashauri waendelee na ushirika hou.
Naye Mwita Waibe kutoka Idara ya
Afya, ustawi wa jamii na Lishe Tamisemi alisisitiza kuwa Ofisi yake inatarajia
kuona ujenzi huo unakamilika ndani ya muda uliopangwa ili kuleta tija na
kuendana na malengo ya mradi huo.Pia alisisitiza kuwa miradi hii itajengwa na
kusimamiwa na kituo hivyo kusisitiza kuchagua mafundi wenye uwezo ambapo
itapelekea thamani ya fedha iendane na ujenzi husika.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri Bw.
Primy Damas aliwahakikishia wajumbe toka Tamisemi kuwa mpaka kufikia mwezi
Aprili 2018, ujenzi utakuwa umekamilika na kuanza kutumika.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni