Zaidi ya wakandarasi 100
wanufaika na semina ya bure toka National Microfinance Bank (NMB) ya namna ya
kushinda zambuni mbalimbali zinazotangazwa hapa nchini.
Akizungumza na wakandarasi hao katika ukumbi wa Idd Nyundo, Mkurugenzi
wa Manispaa ya Temeke Ndugu Nassib Mmbaga aliwataka wakandarasi hao kutumia
nafasi hiyo kuhakikisha wanatumia fursa ilioyotolewa na kujipatia mikopo ili
kuweza kuwa na ushindani pindi fursa zinapotangazwa tenda mbalimbali
zinatangazwa wasisite kuomba kwani hiyo ni fursa pekee ya kujitokeza na
kuonyesha uwezo katika kazi na kampuni husika.
Nae Meneja wa kanda Ndugu Badru
Idd aliwatoa hofu wakandarasi hao na kuwataka wasisite kujitokeza kuomba mikopo
na ushauri toka NMB, ili kuweza kuibuka vinara katika soko la ushindani pindi
zitangazwapo zabuni mbalimbali.
''NMB ni benki ya kizalendo hivyo
msisite kutuona na tufanye mazungumzo ya namna bora ya kusaidiana na kujikwamua
kimaisha, mikopo yetu ni rahisi na yenye riba nafuu kwa mwananchi yoyote
aliedhamiria kujikomboa. Pia tuna matawi mengi karibu kila mahali hapa Dar es
salaam hivyo tumekufikia popote ulipo'' Alisisitiza.
Vile vile alibainisha kwamba
ukiwa na NMB unaweza kupata mikopo na huduma zozote za kielektroniki pamoja na
mikopo mbalimbali, pia alielezea uwepo wa akaunti mbalimbali za biashara mfano
World Wide akaunti, Business Saving akaunti, Fanikiwa akaunti na NMB connect akaunti
ambapo zote hizi ni maalumu kwa wafanyabiashara.
Semina hiyo ya siku moja
ilifanyika ikiwa na lengo madhubuti la kuwasaidia wakandarasi na kuwatoa hofu
ya kuomba mikopo NMB, ili kuwawezesha kushika tenda zinazotangazwa hapa nchini
hususani zilizopo ndani ya Manispaa ya Temeke.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni