Tafuta katika Blogu Hii

Jumamosi, 14 Oktoba 2017

MAADHIMISHO YA KUMBUKUMBU YA NYERERE YAFANA TEMEKE


  Katika kuadhimisha siku ya kumbumbuku ya hayati Baba wa Taifa Mwl; Julius Kambarage Nyerere, Wilaya ya Temeke yafanya michezo mbalimbali ambayo ilijumuisha watumishi wote wa Wilaya hiyo na vilabu vyote vya michezo vya Mkoa wa Dar.
Mgeni rasmi wa tamasha hilo ambaye ni Mkuu wa wilaya ya Temeke Mh:Felix Lyaniva alifurahishwa na kazi nzuri ya maandalizi ya Tamasha hilo, jinsi watumishi na vilabu vya michezo walivyojitokeza kwa wingi katika kuadhimisha siku hiyo ya kifo cha baba wa taifa.
Lyaniva alisisitiza kuyaishi maisha ya Mwl Nyerere  kwa kuawazalendo wa taifa letu na kuikataa rushwa ambayo ni adui wa maendeleo na adui wa haki. Alisema "Mwalimu Nyerere alikua mpenzi wa michezo ndio maana leo tunamuenzi". Mwl Nyerere ndiye alikua muanzilishi wa michezo mbalimbali.

Alisisitiza katika vilabu vyote vya michezo kuwa na shughuli mbalimbali za kijasiliamali ili kujikwamua kiuchumi.Alisema hayo alipowakumbusha wanamichezo kuwa pamoja na kwamba michezo ni afya lakini pia ikitumiwa vizuri itakuinua kiuchumi.


Alifafanua zaidi ikiwa vikundi vya michezo vikiungana na kuamua kufungua viwanda vidogo itasaidia kupata ajira, pesa ,pia itapunguza kundi kubwa la wahalifu. Alimuunga mkono raisi wa awamu ya tano Dr.John Pombe Mgufuli katika jitihada zake za sera ya maendeleo ya ukuaji wa uchumi wa viwada ili kufikia uchumi wa kati. Pia Mh:Lyaniva ahaidi tamasha hili kufanyika kila mwaka, hivyo waandaaji wajipange koboresha michezo yote.
Mgeni rasmi  alishiriki mbio za mwendo mfupi km 5 kuanzia uwanja wa uhuru, pia alifungua bonanza kwa kukimbia na washiriki wengine mbio za mita 100.
Pamoja na hayo tamasha lilipambwa na shangwe za michezo mbalimbali yenye kufurahisha kama kukimbiza kuku,kukimbia na gunia, na kukimbia na kijiko chenye ndimu mdomoni. 


Pia kulikua na upimaji wa afya, magonjwa mbalimbali yalipimwa ikiwamo saratani ya shingo ya kizazi kwa wanawake, shinikizo la damu,kisukari nk
Katika bonanza hilo team zote  za manispaa zimefanya vizuri.
Pia bonanza hilo lilipambwa na wanaskauti wa wilaya ya Temeke,ambao walitoa igizo.
Washiriki wengi walikua na afya njema mpaka mwisho wa tamasha hakukua na majeruhi,kila mtu alionekana kufurahishwa na michezo hiyo.

Ijumaa, 13 Oktoba 2017

SPORTS BONANZA







KATIKA KUAZIMISHA SIKU YA KUMBUKUMBU YA  HAYATI BABA WA TAIFA MWL JULIUS K NYERERE, AMBAPO KILA MWAKA HUKUMBUKWA IFIKAPO 14/10/2017.

MANISPAA YA TEMEKE KWA KUSHIRIKIANA NA VILABU VYA MAZOEZI (TEJA) WAMEANDAA  TAMASHA KUBWA LA MICHEZO, SPORTS BONANZA LITALOFANYIKA KATIKA VIWANJA VYA UHURU KUANZIA SAA 12:30 ASUBUHI. SIKU YA JUMAMOSI.

TAMASHA HILO LITAHUSISHA OFISI YA MKUU WA WILAYA NA WATUMISHI WOTE WA WILAYA HIYO.

MGENI RASMI ATAKUA MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM MH;PAUL MAKONDA



NYOTE MNAKARIBISHWA.

Jumatano, 11 Oktoba 2017

MKUU WA WILAYA ATOA ZAWADI



Ikiwa leo ni siku ya pili tangu mazoezi ya kuelekea kilele cha bonanza la kuadhimisha siku ya kumbukumbu ya Hayati baba wa Taifa Mwl Julius .K. Nyerere kuendelea katika viwanja vya shule ya Secondary Kibasila, watumishi wamejitokeza kwa wingi kwenye mazoezi.

Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mh.Felix Lyaniva nae  akiwa miongoni mwao, ametoa zawadi ya pesa taslimu kwa wanamichezo waliofanya vizuri, ambapo pesa hiyo ilitolewa kwa mshindi wa kwanza na wapili.Zawadi hizo zitaendelea hadi mwisho wa mazoezi.

Mkuu wa Wilaya amesisitiza ushiriki wa kila Mtumishi katika mazoezi bila kukosa. Pamoja na hayo amefurahishwa na jitihada za wafanya mazoezi kuwa ni ya kuridhisha na amesema anatarajia ushindi wa nguvu kwa team zote za watumishi.
Mazoezi hayo yalihudhuriwa na katibu Tawala Wilaya ya Temeke(DAS) Bwn.Hashimu Komba na Wakuu wa Idara.


Mazoezi hayo yanaendelea mpaka Ijumaa katika viwanja vya Kibasila ambapo team zote zinajinoa kikamilifu ili kuwakabili wapinzani wao. Bonanza hilo linatarajiwa kufanyika katika kiwanja cha Uhuru siku ya Jumamosi ya tarehe  14/10/2017 wiki hii.


Pichani ni watumishi wakiwa mazoezini.














Ijumaa, 6 Oktoba 2017

JUKWAA LA WANAWAKE WAJASILIAMALI TEMEKE LAUNDWA

JUKWAA LA WANAWAKE WAJASILIAMALI TEMEKE LAUNDWA

Katibu Tawala Wilaya ya Temeke Bw:Hashimu Komba aunda jukwaa la wanawake wajasiliamali wa wilaya ya Temeke ambao walijitokeza kwa wingi kutoka kata zote za wilaya hiyo. Akiongea na wanawake hao wajasiliamali leo katika ukumbi wa Iddi Nyundo Manispaa ya Temeke.



               Pichani Bw:Hashimu Komba, Katibu Tawala Wilaya ya Temeke.


kauli mbiu ya kikao hicho ni “Mwanamke tumia fursa kuimalisha uchumi wa viwanda” ambapo Katibu tawala huyo ameungana na juhudi za Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu ikiwa ni mwendelezo wa uzinduzi wa jukwaa la wanawake katika kuinua uchumi wa mwanamke ili kuleta Maendeleo ya taifa kiwilaya.
Kauli mbiu hiyo ilisemwa na Makamu wa Rais katika siku ya uzinduzi wa Jukwaa la uwezeshaji wa wanawake kiuchumi kimkoa lililofanyika katika viwanja vya Posta,kijtonyama. Ambapo uzinduzi huo ni wa 23,lililoandaliwa na Baraza la uwezeshaji kwa ufadhili wa benki ya CRDB.
Komba aliwamwagia sifa wanawake kwa juhudi zao za kujikwamua kiuchumi katika jamii,aliwapongeza akina mama kwanamna wanavyojituma na kuwa waaminifu na kuwa na uwezo wa kusimamia vipato vyao vidogo wanavyopata kwa kujileta maendeleo makubwa.



  
 Pichani watumishi wa Manispaa na wanawake wajasiliamali wakimsikiliza        Bw:DAS kwa makini.


Ahadi kuwa jukwaa hilo punde litakopo undwa litakuwa na tija kubwa katika kujitangazia biashara na ubunifu wa kazi zao wanazofanya katika ngazi za kimataifa,kitaifa,kimkoa,kiwilaya mpaka kata. Pia watapata fursa mbalimbali za kupiga hatua kama kushiriki maonesho ya kibiashara ya sabasaba na nanenane. Hivyo asisitiza kuchaguliwa kwa viongozi walio na uwezo wakusimamia mawazo,ubunifu na ujuzi wa kazi zao ili kusimamia jukwaa hilo katika kujiletea maendeleo.

Hata hivyo amewapa moyo kuwa kuelekea katika sera ya uchumi wa viwanda kwa kuanzia waendelea kutumia technolojia hizo hizo ndogondogo wanazotumia nyumbani kuzalisha bidhaa mbalimbali ikiwa ni mfano wa viwanda vidogovidogo,wakati wanajiandaa kupata viwanda vikubwa. Kwakufanya hivyo watakuwa wanajiingizia kipato,pia kuinua uchumi wa viwanda katika nchi yetu.



Wanawake wajasiliamali wakiwa katika kikao cha uundaji wa jukwaa la wanawake wajasiliamali kiwilaya.


Katika kikao hicho katibu Tawala huyo alipongeza Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii inayoongozwa na John Bwana kwa kazi nzuri wanayoifanya kwa kuwatambua wajasiliamali hao ambao wamejitokeza kwa wingi na shauku kubwa kuunda jukwaa hilo.

Jukwaa hilo linatazamiwa kuzinduliwa hivi karibuni lengo kuu ikiwa ni kumwinua mwanamke kufikia katika uchumi wa kati, ambapo inasemekana mwanamke ni mlezi wa familia na jamii, ukimwezesha mwanamke imeliwezesha taifa.
Top of Form


TEMEKE BILA UCHAFU INAWEZEKANA.

MKUU WA WILAYA YA TEMEKE APOKEA MAPIPA ZAIDI YA 241 KWA AJILI YA KAMPENI YA “TEMEKE BILA UCHAFU INAWEZEKANA” Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mh F...