Ikiwa leo ni siku ya
pili tangu mazoezi ya kuelekea kilele cha bonanza la kuadhimisha siku ya
kumbukumbu ya Hayati baba wa Taifa Mwl Julius .K. Nyerere kuendelea katika
viwanja vya shule ya Secondary Kibasila, watumishi wamejitokeza kwa wingi
kwenye mazoezi.
Mkuu wa Wilaya ya
Temeke Mh.Felix Lyaniva nae akiwa
miongoni mwao, ametoa zawadi ya pesa taslimu kwa wanamichezo waliofanya vizuri,
ambapo pesa hiyo ilitolewa kwa mshindi wa kwanza na wapili.Zawadi hizo
zitaendelea hadi mwisho wa mazoezi.
Mkuu wa Wilaya
amesisitiza ushiriki wa kila Mtumishi katika mazoezi bila kukosa. Pamoja na
hayo amefurahishwa na jitihada za wafanya mazoezi kuwa ni ya kuridhisha na
amesema anatarajia ushindi wa nguvu kwa team zote za watumishi.
Mazoezi hayo
yalihudhuriwa na katibu Tawala Wilaya ya Temeke(DAS) Bwn.Hashimu Komba na Wakuu
wa Idara.
Mazoezi hayo
yanaendelea mpaka Ijumaa katika viwanja vya Kibasila ambapo team zote zinajinoa
kikamilifu ili kuwakabili wapinzani wao. Bonanza hilo linatarajiwa kufanyika
katika kiwanja cha Uhuru siku ya Jumamosi ya tarehe 14/10/2017 wiki hii.
Pichani ni watumishi wakiwa mazoezini.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni