Tafuta katika Blogu Hii

Jumamosi, 14 Oktoba 2017

MAADHIMISHO YA KUMBUKUMBU YA NYERERE YAFANA TEMEKE


  Katika kuadhimisha siku ya kumbumbuku ya hayati Baba wa Taifa Mwl; Julius Kambarage Nyerere, Wilaya ya Temeke yafanya michezo mbalimbali ambayo ilijumuisha watumishi wote wa Wilaya hiyo na vilabu vyote vya michezo vya Mkoa wa Dar.
Mgeni rasmi wa tamasha hilo ambaye ni Mkuu wa wilaya ya Temeke Mh:Felix Lyaniva alifurahishwa na kazi nzuri ya maandalizi ya Tamasha hilo, jinsi watumishi na vilabu vya michezo walivyojitokeza kwa wingi katika kuadhimisha siku hiyo ya kifo cha baba wa taifa.
Lyaniva alisisitiza kuyaishi maisha ya Mwl Nyerere  kwa kuawazalendo wa taifa letu na kuikataa rushwa ambayo ni adui wa maendeleo na adui wa haki. Alisema "Mwalimu Nyerere alikua mpenzi wa michezo ndio maana leo tunamuenzi". Mwl Nyerere ndiye alikua muanzilishi wa michezo mbalimbali.

Alisisitiza katika vilabu vyote vya michezo kuwa na shughuli mbalimbali za kijasiliamali ili kujikwamua kiuchumi.Alisema hayo alipowakumbusha wanamichezo kuwa pamoja na kwamba michezo ni afya lakini pia ikitumiwa vizuri itakuinua kiuchumi.


Alifafanua zaidi ikiwa vikundi vya michezo vikiungana na kuamua kufungua viwanda vidogo itasaidia kupata ajira, pesa ,pia itapunguza kundi kubwa la wahalifu. Alimuunga mkono raisi wa awamu ya tano Dr.John Pombe Mgufuli katika jitihada zake za sera ya maendeleo ya ukuaji wa uchumi wa viwada ili kufikia uchumi wa kati. Pia Mh:Lyaniva ahaidi tamasha hili kufanyika kila mwaka, hivyo waandaaji wajipange koboresha michezo yote.
Mgeni rasmi  alishiriki mbio za mwendo mfupi km 5 kuanzia uwanja wa uhuru, pia alifungua bonanza kwa kukimbia na washiriki wengine mbio za mita 100.
Pamoja na hayo tamasha lilipambwa na shangwe za michezo mbalimbali yenye kufurahisha kama kukimbiza kuku,kukimbia na gunia, na kukimbia na kijiko chenye ndimu mdomoni. 


Pia kulikua na upimaji wa afya, magonjwa mbalimbali yalipimwa ikiwamo saratani ya shingo ya kizazi kwa wanawake, shinikizo la damu,kisukari nk
Katika bonanza hilo team zote  za manispaa zimefanya vizuri.
Pia bonanza hilo lilipambwa na wanaskauti wa wilaya ya Temeke,ambao walitoa igizo.
Washiriki wengi walikua na afya njema mpaka mwisho wa tamasha hakukua na majeruhi,kila mtu alionekana kufurahishwa na michezo hiyo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

TEMEKE BILA UCHAFU INAWEZEKANA.

MKUU WA WILAYA YA TEMEKE APOKEA MAPIPA ZAIDI YA 241 KWA AJILI YA KAMPENI YA “TEMEKE BILA UCHAFU INAWEZEKANA” Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mh F...